HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2022

TAIFA STARS KUWAFUATA LIBYA USIKU MNENE


Timu ya Taifa “Taifa Stars” itaondoka kesho Jumanne alfajiri kuelekea Libya kwa michezo ya Kirafiki kwenye Kalenda ya FIFA.

Stars watakuwa na kibarua kizito katika mitanange miwili dhidi ya Timu ya Taifa ya Libya katika kalenda ya FIFA mwishoni mwa juma hili.

Kama Stars itafanikiwa kufanya vizuri katika michezo hiyo itaiwezesha kupanda kwenye viwango vya ubora wa FIFA.

Lakini pia michezo hiyo itakuwa kipimo kingine kwa Kocha Honour Janza na Benchi lake la Ufundi kwa namna wanavyoendelea kukifuma upya kikosi hicho baada ya kuondoshwa kwenye kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani CHAN.

Msafara wa Stars utawasili Uwanja wa Ndege JNIA saa 8 usiku kuanza safari hiyo wenye kikosi cha wachezaji 23.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni

Aish Manula, Beno Kakolanya, Said Kipao, Kibwana Shomary, Darius Peter, David Luhende, Abdurmalick Adam, Abdi Banda, Carlos Protas, Oscar Masai, Dickson Job, Abdallah Mfuko, Himid Mao, Sospeter Bajana, Mzamiru Yassin, Feisal Salum, David Uromi, Mohamed Banka, Mbwana Samatta, Simon  Msuva, Ibrahim Joshua, Said Hamis na Habib Kyombo.

No comments:

Post a Comment

Pages