HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2022

TIMU YA TAIFA SOKA LA UFUKWENI KUANZA KIBARUA KESHO COSAFA


Na Mwandishi Wetu

Timu ya Taifa Soka la Ufukweni imewasili salama nchini Afrika Kusini asubui ya leo tayari kwa Fainali za COSAFA za mchezo huo.

Baada ya kuwasili Wachezaji wa Timu ya Taifa Soka la Ufukweni wakiwa chini ya Kocha Mkuu Boniface Pawasa wamefanya matembezi katika fukwe za South beach Arena ambako ndiko mashindano yatafanyika.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na timu shiriki ni Mataifa nane yaliyogawanywa katika makundi mawili.

KUNDI A, Mozambique, Senegal, Seychelles na South Africa.

KUNDI B. Tanzania, Uganda, Egypt na Mauritania.

Kikosi kilichowasili Afrika Kusini tayari kwa mashindano hayo yanayoanza kutimua vumbi hapo kesho ni pamoja na.

Adam Hamis, Ahmed Rajabu, Ibrahim Hamidu, Shaban Hassan, Erick Manyama, Ismail Gambo , Juma Sultan, Mtoro Nassoro.

Wengine ni Stephano Nkomola, Sadick Rajabu, Jaruph Rajab Ibrahim Ibadi, Goodluck Gama, Yahya Tumbo Stephano Mapunda na Abdallah Mohamed.

No comments:

Post a Comment

Pages