HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 19, 2022

AZAM WAMPATA 'MRITHI' WA ZAKA ZAKAZI


 

Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Klabu ya Azam FC imemtangaza aliyekuwa Mtangazaji wa  kituo cha Tv cha Azam TV Hashim Ibwe, kuwa Ofisa Habari wa Klabu hiyo wa muda.

Taarifa hiyo imetolewa jioni ya leo, ambapo imebainisha kuwa Ibwe atakuwa Ofisa Habari wa muda wakati huu ambao Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Thabiti Zakaria aliitumikia adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na Mchezo wa Mpira wa Miguu kwa miezi mitatu.

Zakaria alikumbana na adhabu hiyo baada ya Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu maarufu kama masaa 72 kumkuta na hatia ya kuwatuhumu waamuzi wa Ligi Kuu kutoitendea haki klabu hiyo katika michezo mbalimbali ya Ligi jambo ambalo ni kinyume cha Maadili kwa viongozi wa Klabu na wanachama wa Ligi husika.

Taarifa hiyo imeeleza Ibwe atashika nafasi hiyo kwa muda huo wa miezi mitatu na baada ya hapo klabu itatoa taarifa juu ya mustakabali wa kuendelea na Ibwe ama vinginevyo.

No comments:

Post a Comment

Pages