Na Mwandishi Wetu
Klabu Africain ndio timu ya pili kwa ukubwa na mafanikio makubwa nyuma ya klabu ya Esparance Sportive de Tunis nchini Tunisia.
Club Africain ilianzishwa mwaka 1920 huku Esparence Sportive de Tunis ikianzishwa mwaka 1919.
Katika mafanikio ya ligi ya ndani inashika nafasi ya pili ikiwa ina jumla ya mataji rasmi 39 nyuma ya Esparence wakiwa na mataji rasmi 53.
Kwenye ligi kuu ya nchini Tunisia Club Africain ametwaa jumla ya mataji 13 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Esparence wenye jumla ya mataji 32 wakiwa ndio vinara wa mataji katika ligi hiyo.
Kwenye mafanikio ya kimataifa Club Africains wamewahi kuwa mabingwa wa ligi ya mabingwa barani Afrika katika msimu wa mwaka 1991 wakiwafunga SC Villa ya nchini Uganda kwa jumla ya mabao 7-2 mechi zilichezwa mbili nyumbani na ugenini,ugenini ilikuwa sare 1-1 na nyumbani Cluba Africains walishinda mabao 6-1.
Kwenye historia ya kombe la Shirikisho hawajawahi kubeba ubingwa wa michuano hiyo lakini waliwahi kufika fainali mwaka 2011 na kufungwa kwa penati 6-5 na klabu ya Maghreb Association Sportive de Fès ya nchini Morocco.
Licha ya historia kubwa ya timu hiyo,wamekuwa na rekodi mbaya kwani wameshindwa kubeba kombe lolote tangu msimu wa mwaka 2018 walipobeba ubingwa wa kombe la Tunisia(Sio ligi kuu).
Mara ya mwisho kubeba ubingwa wa ligi kuu ilikuwa katika msimu wa mwaka 2015 na kuanzia hapo hawajawahi kumaliza hata katika nafasi ya pili katika ligi hiyo,yote hayo yanatokana na anguko kubwa la kiuchumi ndani ya timu hiyo.
Msimu uliopita walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 4.
Club Africain wanatumia Uwanja wa Stade Olympique De Rades unaochukuwa watazamaji 60,000 kama ulivyo Uwanja wa Taifa.
Club Africain wamepangwa kukutana na Yanga katika michezo ya kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza utapigwa Dar es Salaam Young Africans wakiwa wenyeji huku mchezo wa mkondo wa pili ukipigwa Novemba 9 mjini Tunis nchini Tunisia.
Ikumbukwe kuwa Club Africain ndio wamewaondoa Kipanga FC kwa kipigo kizito cha mabao (7-0), mchezo wa kwanza pale Zanzibar walitoka Suluhu kisha kusinda (7-0) mchezo wa mkondo wa pili pale Tunis.
October 19, 2022
Home
Unlabelled
HII NDO CLUB AFRICAIN WAPINZANI WA YANGA SHIRIKISHO
HII NDO CLUB AFRICAIN WAPINZANI WA YANGA SHIRIKISHO
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment