Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Sukari nchini (SBT) Filbert Mponzi akiwa ameongozana na Wajumbe wa Bodi hiyo pamoja na Menejimenti ya kiwanda cha sukari cha TPC walipotembelea moja ya mashamba yaliyokuwa yakivunwa Muwa.
Wajumbe wa Bodi ya Sukari nchini (SBT) pamoja na menejimenti ya kiwanda cha sukari cvha TPC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea moja ya mashamba ya miwa yaliyopo katika eneo la kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Sukari nchini (SBT), Filbert Mponzi (katikati), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu msaidizi upande wa kiwanda Nizam Codabux wakati wajumbe wa bodi hiyo walipotembelea kiwanda cha Sukari cha TPC kujionea shughuli za uzalishaji pamoja na kilimo zinavyofanyika kiwandani hapo. Kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Prof. Kenneth Bengesi. (NA MPIGA PICHA WETU).
Na Mwandishi Wetu
Bodi mpya ya wakurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) imeliahidi taifa neema ya sukari ndani ya miaka mitatu ijayo huku mwenyekiti wake, Filbert Mponzi, akisema tatizo la upungufu wa bidhaa hiyo sasa linaenda kuwa historia.
Mkurugenzi Mkuu wa SBT, Prof Kenneth Bengesi, alisema taifa sasa hivi linabiliwa na nakisi ya tani 60,000 za sukali tatizo ambalo kwa hesabu za kawaida kulitatua kwake ifikapo mwaka 2025 kunahitaji ongezeko la uzalishaji wa wastani wa tani 20,000 kwa mwaka.
Wakizunguma wiki iliyopita huko Moshi, wajumbe hao walisema kuwa tayari taifa lina kila kitu kinachohitajika ili kufikia lengo kuu la sukari la nchi na kupelekea bidhaa hiyo kupatikana kwa urahisi.
Hii ni pamoja na kuwepo sera wezeshi, kukua kwa uzalishaji, ambao takwimu za SBT uliongezeka kwa karibu asilimia 17 ndani ya miaka sita kuanzia mwaka 2013. Pamoja na ukuaji huu,uitaji wa sukari ni mkubwa kuliko kiasi kinachozalishwa na kusambazwa.
Bw Mponzi alisema jithada za kuongeza uwezo wa uzalishaji wa sukari wa ndani zinahitaji uboreshaji zaidi mazingira ya biashara ya sekta hiyo ili kuziimarisha miradi ambayo tayari ipo na kuwavutia wawekezaji wapya.
Bw. Mponzi alisema jitihada za kuongeza uwezo wa uzalishaji wa ndani zitahitaji uboreshaji zaidi wa mazingira ya biashara ya sekta hiyo ili kuunganisha eneo la uendeshaji na kuvutia wawekezaji wapya.
Kama kiogozi wao, wajumbe wa bodi ya SBT walitilia mkazo wa Tanzania nayo kuanza kuuza sukari nje ya nchi kwani uwezo wa kufanya hivyo inao kiasi cha kuweza kuwa kigogo wa biashara hiyo kwenye eneo hili.
“Wakati anaizindia bodi hii, Waziri wa Kilimo, Bw Hussein Bashe, alitupa maelekezo zaidi ya kumi ya kimwongozo hata hivyo alisisitiza jambo moja kwamba ni lazima bodi hii mpya ihakikishe kuwa taifa linajitosheleza kwa sukari ifikapo mwaka 2025,” Bw Mponzi aliwaambia waandishi wa habari wakiwa kwenye kiwanda cha sukari cha TPC Moshi.
“Hili ndilo lengo letu kuu na kipaumbele cha Serikali, ambalo linaweza kufikika kama tutakuwa na sera wezeshi na kuyaweka sawa yale mambo yote yanayokwaza kukua kwa sekta hii,” mwenyekiti huyo alibainisha wakati wa ziara yao ya kikazi kwenye kiwanda cha TPC Jumanne baada ya kukutana kwa mara ya kwanza jijini Arusha.
Mkutano huo wa siku tatu ulihudhuliwa na wajumbe wake sita kati ya nane. Mbali na mwenyekiti Mponzi, wengine waliokuwepo ni pamoja na Ephraim Balozi Mafuru, Hussein Suphian Ally, Pelagia Zacharia Kayonga, MPaulo Matiko Chacha and Jitihada Yusuph Chelenzo.
“Tukipata ushirikiano wa wadau wote na miradi inayoendelea kuongeza uwezo wa kuzalisha kama huu hapa wa kupanua mashamba ya miwa uhaba wa sukari muda si mrefdu utakuwa historia,” Mponzi aliongeza.
Maendeleo ya uchumi wa sukari nchini ni moja ya vipaumbele vya kilimo vya serikali kukabilina na ongezeko la uitaji wa sukari kwenye soko la ndani.
Prof Bengesi aliserma mienendo kadha kwenye sekta inaashilia kuwepo kwa mafanikio mazuri katika hilo huku serikali ikiipa bodi mpya ya SBT jukumu la kuhakikisha azma ya taifa ya kuzajitosheleza kwa sukari inatimia ifikapo mwaka 2025.
Mwenendo huu chanya unawekwa wazi na kuonekana vizuri na takwimu alizozibainisha kiongozi huyo wa SBT zilizoonyesha kuwa uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka hadi tani 380000 lakini hata hivyo bado mahitaji nayo ni makubwa yakifikia tani 440,000 ;’
“Ziara hii ya wajumbe wa bodi TOC and nyingine watakazozifanya ni kwa ajili ya kuwapa nafasi kuanza kuijua tasnia wakijiandaa kutekeleza majumu yao,” Prof Bengesi alisema.
“Sisi kama wadhibiti, tuna jukumu la kusimamaia maendeleo ya tasnia na kusadia kuzikabili dosari zinazoikwamisha kama sehemu ya msukumo mpya wa serikali wa kuiendeleza sekta na kulifanya soko litangamae,” alifafanua.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Bw Marius Jacobs alisema sekta kwa sasa imekuwa inakua vizuri na kuwawezesha wazalishaji kuzalisha zaidi ili wasaidie kupunguza changamoto ya kuagiza sukari nje.
Bw Jacobs alisema uwekezaji huo umekuwa wa tija kwani umeimarisha uzalishaji kitaifa na kwa kampuni hiyo hadi tani 110,000.huku matarajio yakiwa ni kuongezeka hadi tani 115,000 mwaka 2025.
Sukari inayozalishwa nchini nangu kampuni hiyo ibinafsishwe tayari wamewekeza zaidi ya 250bn/-kukarabati mitambo, kuongeza uzalishaji and kukiendesha kiwanda kisasa zaidi.ilioongezeka kwa asilimia 16.6 kutoka tani 307,431 hadi tani 359,219 kati ya mwaka 2013 na 2019 kabla ya kufikia 367,000 mwaka jana.
No comments:
Post a Comment