HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 16, 2022

SIMBA; TWENDE KHARTOUM AMA MNASEMAJE?

 


Na John Richard Marwa


Ukiwa na jeuri unaweza ifanya Dunia nzima iwe yako ukitaka lolote itatii amri yako, Ndivyo ambavyo Simba hunafanya kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.


Simba anatinga tena hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kwa kuwaondosha De Agosto kwa jumla ya mabao (4-1) baada ya dakika 90 za pili kutamatika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkap jioni ya Leo.


Alikiwa ni Moses Phiri 'Jenerali' kwa mara nyingine akifunga bao lake la tano msimu huu katika michezo minne ya kutinga hatua ya makundi.


De Agosto walikuja kiume kweli kweli kwa kuja na mpango mkakati wa kuwazuia Simba kwa kuwanyima nafasi ya kutengeneza mashambulizi yao katikati ya mstari wa ulinzi na kiungo.


Ubora wa Simba ulifia hapo nankulazimika kutumia mipira ya juu kwa kuutanua Uwanja kumtafuta Agustin Okrah na Pape Sakho.


Simba ilihitaji ubora wa tukio moja kuuwa mchezo na likapatikana kutoka kwa Jenerali akipokea pasi kutoka kwa Mohamed Hussein 'Zimbwejr'.


Kipindi cha pili Simba walirejea kwa kuutuliza mchezo wakikaba kwa namba kumbwa na kiwaruhusu De Agosto kucheza kwenye eneo lao.


Hii ni mara ya nne katika misimu mitano Simba wanatinga hatua ya makundi kwenye michuano ya Afrika.


Simba wanaungana na miamba mingine Afrika kutinga hatua hiyo ya makundi huku michezo mingine ikitarajiwa kupigwa usiku wa Leo.


Watani wa jadi wa Simba SC, Yanga SC watashuka dimbani usiku wa leo kuwakabili Al Hilal katika Uwanja wa Ounduman Khartoum nchini Sudan, Simba wasafari kuwapa Nguvu Yanga ? 

No comments:

Post a Comment

Pages