HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2022

NGOMA IMELIA, MVINYO UMENYWEKA LUPASO

 


Na John Marwa

HATIMAYE ngoma imelia na mvinyo umenywekwa ndani ya Dimba la Benjamin Mkapa kwa Dodoma Jiji kukubali kipigo cha mabao (3-0) kutoka kwa Simba SC.

Ulikuwa mchezo mgumu kwa walima zabibu wa Dodoma Jiji mapena tu kupitia kwa mlinzi wake Abdallah Shaibu Ninja kujifunga baada ya krosi iliyomiminwa na Clatous Chama.

Bao hilo ni kama lilizima mpango wa Simba SC waliokuja nao katika mtanange wa leo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NPL wa kusaka ushindi na kuendeleza mdundo wa kutopoteza mchezo .

Kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwa vijana wa Masoud Djuma kwani kila gia waliojaribu kuingiza ni kama swichi kwa wanajeshi wa Juma Mgunda kuendeleza maangamizi.

Dodoma Jiji walikuwa bora katika kujilinda nankaunzisha mashambulizi katika mfumo wa 3:5:2 lakini ubora wa Simba eneo la katikati lilikuwa katika kuziba nafasi na kufungua nafasi ulikuwa unawafanya Dodoma Jiji kuacha mianya pale walipokuwa wanapoteza mpira.

The General Moses Phiri aliendeleza wimbi lake la kufumania nyavu kwa kaundika Bao la nne msimu huu katika michezo mitano aliyoshuka Dimbani.

Super Sub Habib Kyombo aliandikia Simba bao la tatu na la ushindi akimalizia krosi mujarabu kutoka kwa Mohamed Hussein.

Ushindi huo unaifanya Simba kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa kufikisha point 13 na mabao 11 ya kufunga, clean sheets 4 huku wakiwa wameruhusu mabao 2 kwenye mchezo mmoja dhidi ya KMC FC.

Ligi hiyo itaendelea kesho kwa Mabingwa watetezi kushuka dimbani kuwakabili Ruvu Shooting. Azam FC wao watawakalibisha Singida Big Stars.

No comments:

Post a Comment

Pages