Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Amebainisha
kuwa Sera ya Nishati ya 2015 inayosimamiwa na wizara hiyo inaelekeza
Wizara kuchukua hatua za kuwawezesha watanzania kupata nishati safi na
salama na kwa gharama wanayoimudu ili kuboresha ustawi wa watanzania kwa
kiasi kikubwa.
Amesisitiza kuwa mjadala huo utaratibiwa na wizara hiyo ili kupata majibu ya kudumu ya kuondokana na matumizi ya nishati ya kupikia ya mkaa na kuni nchini pamoja na kupata uelewa wa pamoja juu ya suala nishati ya kupikia hapa nchini.
Ameongeza kuwa katika mkutano huo watangazia katika mlengo wa kiuchumi, kijinsia, afya, usawa na mazingira kwa namna ambavyo tunapika hapa nchini kwa kutumia nishati safi na salama.
Waziri Makamba amesema mjadala huo utapelekea kutambua changamoto za kutumia kuni na mkaa, athari zilizopo na kuangalia matokeo yake ni nini.
Amefafanua kuwa mifumo ya Kisera Sheria, Kikodi, Kifedha na Utawala itawekwa kwa ajili ya kupambana na hali ya namna tunavyopika na kuwaondoa watanzania kutumia nishati inayoathiri afya na maisha.
Akizungumzia kuhusiana na madhara yanayojitokeza katika jamii juu ya matumizi ya kuni, mkaa na nishati nyingine zisizo safi na salama Waziri Makamba amesema Vituo vya afya Nchini vimeelemewa na mzigo mkubwa wa utoaji huduma za afya za mfumo wa upumuaji zinazotokana na namna tunavyopika kwa kutumia nishati zisizosafi na salama.
Pa amesema Watanzania zaidi ya 33,000 wanafariki dunia kwa mwaka kutokana na kuvuta moshi wa namna tunavyopika chakula hivyo hii inaendelea kuathiri akina mama na watoto wa kike kwa kupoteza muda mwingi kwenye kutafuta nishati ya kupikia ya kuni.
“Wanapokuwa
wanatafuta nishati hiyo wanapunguza muda wa kutafuta elimu au kufanya
shughuli nyingine za uzalishaji mali huko polini wanakutana na dhahama
na matukio ya unyanyasaji wa kijisia.
Pia Nishati isiyo safi na salama inaleta utofauti au kutokuwa na usawa kati ya wanawake na wanaume, watu wa mjini na vijijini wenye kipato na wasio na kipato.” Amesema Waziri Makamba
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Seif Saidy amesema mkutano huo utajadili kwa namna gani matumizi ya nishati zisizo safi zinavyoathiri afya za watanzania na kuja na majibu yatakayofanikisha kupatikana kwa nishati safi na salama ambazo wananchi watazimudu.
Nae,Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Pauline Chale ameeleza kuwa matumizi ya Nishati isiyo safi na salama inasababisha changamoto nyingi hasa katika afya na matibabu yake ni gharama kubwa
Dkt. Pauline amesema kuwa magonjwa wa mfumo wa upumuaji yanaondoa uhai wa watu na kwamba matumizi ya kuni, mkaa na mavi ya wanyama yanasumu zaidi ya 200 ndio maana watu wengi wanakuwa na macho mekundu kutokana na sumu hizo zinazopatikana kwenye moshi.
No comments:
Post a Comment