RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ya kuhitimisha kisomo
cha Hitma ikisomwa na Sheikh Mussa Ali Kirobo.(hayupo pichani) kumuombea
Marehemu Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini kilichofanyika katika Msikiti wa Ijumaa
Bweleo Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 23-10-2022, na (kulia kwa Rais)
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume na
(kushoto kwa Rais) Mwalimu Khamis.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini, baada ya kumalizika kwa kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Bweleo Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 23-10-2022. (Picha na Ikulu).


No comments:
Post a Comment