HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 23, 2022

WATANI WATULIZANA BOLI

 


Mshambuliaji wa Simba, Augustine Okra akiifungia timu yake bao baada ya kumpiga tobo kipa wa Yanga, Djigui Diarra katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zimeenda mapumziko uku zikiwa zimefungana bao 1-1.

Mshambuliaji wa Simba Augustine Okra akiwaongoza wachezaji kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga unaofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zimeenda mapumziko uku zikiwa zimefungana bao 1-1.



Na Mwandishi Wetu

Hatimaye dakika 90 za hakuna mbambamba zimekamilika kwa Yanga SC kutoshana nguvu dhidi ya Simba SC kwa sare ya bao (1-1).

Kwa uwiano wa dakika zote 90, matokeo ya sare ni sawa kwa kila mmoja , timu zote mbili zilikosa utulivu katika nyakati muhimu sana , pengine ni presha ? Kutaka kukusanya ujiko ? Ubora ? Wachezaji wenyewe wana majibu ya kutoa

Simba na Yanga mifumo yao haikutufoatiana ni 4-2-3-1 lakini utofauti ni katika uchezaji hasa mawinga wa pembeni ... kivipi.

Moloko na Kisinda walikuwa pembeni sana wanatanua uwanja kupita nyuma na nje ya mafullback wa Simba (Israh na Zimbwe) maana yake walitaka mafullback wa Simba wasibane ndani , waache gap baina yao na mabeki wa kati

Sakho na Okrah walikuwa wanaombea mipira ndani zaidi ( half spaces zote za kulia na kushoto ) ili kuwavuta Kibwana na Djuma ndani na kuwapa nafasi Zimbwe na Israh ku overlap juu zaidi na walifanya hivyo wakijua mawinga wa Yanga walikuwa wanachelewa kurudi nyuma kuzuia au hawarudi kabisa kwahiyo inakuwa rahisi pembeni ya uwanja Simba kutengeneza 2Vs1
Yani ( Okrah na Zimbwe Vs Djuma na Sakho na Israh Vs Kibwana )

Kipindi cha pili Yanga walianza mechi vizuri walikuwa haraka, walitulia katika kumiliki mpira na walifika haraka kwenye kuwania mpira , pongezi kwa Mgunda aliona hilo kwamba Dick na Bangala wanapata nafasu kubwa ya kuanza mpira akabadilisha kuingia kwa Kyombo na umbo la Simba bila mpira ilikuwa 4-4-2 ( Kyombo na Phiri mbele ) na wakiwa na mpira ni 4-2-3-1 , Phiri kwenye namba 10 , Chama pembeni kushoto

Baada ya maelekezo yote kutoka kwa Walimu wachezaji wa pande zote mbili kuna muda ulikuwa unaona kama wamekubali sare , wachezaji kwenda mbele wachache , hakuna utulivu , Nguvu ya kupushi  imeshuka , ufanisi wa kiwango cha chini.

Pasi ya Chama Jr kwenda kwa Okrah ilikuwa hatari sana na huu ni ubora wa mchezaji kuwa na jicho la kuusoma mchezo.

Bao la mkwaju wa Aziz Ki .. hakuna namna yoyote Manula anaokoa ilikuwa ni ubora wa mpigaji mara baada ya Manula kufanya kila kitu kwenye kuupanga ukuta.

Simba SC wanabaki kileleni mwa msimamo na Yanga wanaendeleza rekodi yao ya kutofungwa kwenye Ligi mchezo wa 43.

No comments:

Post a Comment

Pages