HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 05, 2022

RIPOTI: DAR ES SALAAM INAWEZA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA HEWA CHAFU KUTOKA KATIKA SEKTA YA TAKA KWA ASILIMIA 65 KUPITIA MIKAKATI YA TAKA SIFURI

.Sekta ya uzimamizi wa taka sifuri inaweza kutengeneza ajira zaidi ya kazi 18,000 jijini

.Ulimwenguni, usimamizi bora wa taka unaweza kupunguza uzalishaji wa jumla kwa asilimia 84 (tani bilioni 1.4) na kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji katika sekta zingine.

.Eyes on Africa kama mwenyeji wa COP27 Misri inapanga kuzindua Mpango wa 50 kwa 2050. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nipe Fagio, Ana le Rocha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni ikiwa ni njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani.

 

NA MWANDISHI WETU

 

Kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni utakuwa mojawapo ya njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani na kufikia chini ya nyuzi 1.5° ya ongezeko la joto, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Global Alliance for Incinerator Alternatives (GAIA).
Ripoti iligundua kuwa kupitia mikakati taka sifuri, ifikapo mwaka 2030 Dar es Salaam, Tanzania inaweza kufikia upunguzaji wa gesi chafuzi kwa asilimia 65 kutoka katika sekta ya taka.


Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lenye makao yake makuu nchini Tanzania, Nipe Fagio, Ana le Rocha alisema, "Taka sifuri jijini Dar es Salaam inatoa fursa ya kukabiliana na tofauti za kihistoria za kijamii, zilizowazi kwamba jamii nyingi za kipato cha chini katika jiji hilo hazina huduma za usimamizi wa taka. mapambano na athari za kiafya na kiuchumi za uchafuzi utokanao na taka. 

 

Kupitia njia ya taka sifuri, makundi yaliyo katika mazingira hatarishi- kama vile wanawake, vijana, wakusanya taka wasio rasmi na wenyeji i- yanajumuishwa katika utatuzi wa changamoto ya usimamizi wa taka, na kuleta mabadiliko chanya ya kimfumo katika sekta ya taka ambayo yatajenga msingi wa jiji linastohimili hali ya hewa na lenye usawa."


Haya yanajiri wakati Misri ikijiandaa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP 27) la 2022 mwezi Novemba, ambapo taka itakuwa mojawapo ya ajenda kuu za hali ya hewa kwa bara la Afrika–Misri inapanga kuweka mbele Mpango wa 50 kwa 2050, unaolenga kutibu na kuchakata asilimia 50 ya taka zinazozalishwa barani Afrika ifikapo 2050, juhudi ambazo hazijawahi kufanywa na zenye matarajio makubwa.


“Katika ngazi ya kimfumo, AfÅ•ika ina uwezo mkubwa wa kupiga hatua kuelekea ulimwengu usio na taka kutokana na asilimia kubwa ya viumbe hai, sheÅ•ia inayoendelea juu ya plastiki na kuwepo kwa waokota taka katika miji barani kote. 

 

Kwa sababu zinazowezesha, kama vile uchambuzi wa taka kwenye vyanzo, usimamizi tofauti wa taka hozo, ujumuishaji wa waokota taka na utekelezaji bora wa sheria zilizopo za plastiki, Afrika inaweza kuwa eneo ambalo linaonyesha utekelezaji mzuri wa mifumo ya Taka Sifur," alisema Niven Reddy. Mratibu wa Kanda ya Afrika wa GAIA.


Ripoti ya GAIA ilitoa mfano wa upunguzaji wa hewa chafu kutoka kwa miji minane kote ulimwenguni. Waligundua kuwa kwa wastani, miji hii inaweza kupunguza uzalishaji wa hewa chafu katika sekta ya taka kwa asilimia 84 kwa kuanzisha sera bora za usimamizi wa taka kama vile kutenganisha taka, kuchakata tena,na kutengeneza mboji, kupunguza uzalishaji wa jumla kutoka kwa sekta ya taka kwa zaidi ya tani bilioni 1.4, sawa na uzalishaji wa kila mwaka wa magari milioni 300.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nipe Fagio, Ana le Rocha, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa Taka Sifuri katika miji yote ulimwenguni ikiwa ni njia za haraka na nafuu zaidi za kupunguza joto duniani. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Nipe Fagio, Olary Tomito. (NA MPIGA PICHA WETU).

No comments:

Post a Comment

Pages