Kila ifikapo tarehe 11 ya mwezi Oktoba kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya Mtoto wa Kike. Siku hii imewekwa makhususi ikilenga kuleta uelewa kwa jamii na watu wote duniani juu ya umuhimu na thamani ya kulindwa na kuhakikishiwa haki anazostahiki mtoto wa kike popote alipo duniani.
Haki na stahiki hizo ni pamoja na kupatiwa malezi bora, elimu, afya, hifadhi na uwezeshwaji katika kutimiza ndoto na malengo yake.
Siku hii pia ni kielelezo cha kujenga taswira mpya na kupigania mageuzi ya kisera, kisheria na kimkakati ili mtoto wa kike apate mafunzo, haki na stahiki nyinginezo kutoka kwa wazazi, jamii, serikali na wadau wengine. Ni siku inayotumbusha kuungana katika kutetea kupatikana haki na ustawi bora wa mtoto wa kike.
Ni kutokna na msingi huo, Umoja wa Mataifa uliona haja wa kuwepo na siku hii ili kuzitaka serikali za nchi zote duniani, wakiwemo watunga sera, wadau na wahusika wote kuhakikisha wanawekeza vya kutosha katika kupatikana, kulinda, kuhifadhi na kuendeleza haki za Mtoto wa Kike Duniani.
Hatua hiyo itaongeza uwezo na thamani ya mtoto wa kike popote alipo na kumuwezesha kumudu maisha yake na kuondokana na vikwazo mbalimbali katika kupata elimu, makuzi bora, afya stahiki na mahitaji yake muhimu na ya msingi katika makuzi na ustawi wake.
Kwa upande wetu Chama cha ACT Wazalendo, tukiwa taasisi ya wananchi na umma kwa ujumla tunaungana na watu wote duniani katika maadhimisho ya siku hii muhimu ya Mtoto wa Kike Duniani.
Aidha, kama Chama tunaamini kuwa tuna haki na wajibu wote kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki na stahiki zote za mtoto wa kike wa ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ustawi wa mtoto wa kike ni kipaumbele chetu kama Chama cha watu, kinachosimamia na kupigania masuala ya watu.
Chama chetu kiko katika rekodi za kupigania na kutetea haki, maslahi na stahiki za mtoto wa kike.
Kiongozi wa Chama Ndg. Zitto Zuberi Kabwe ni mfano halisi wa mapambano ya haki za mtoto wa kike.
Tarehe 22 Januari, 2020 aliandika barua rasmi Benki ya Dunia akiitaka taasisi hiyo kubwa ya kifedha duniani kutoifadhili Tanzania katika elimu kwani Serikali ililenga kuutumia ufadhili huo kuendelea ubaguzi wa watoto wa kike na kukiuka haki za watoto wa kike kupata elimu bila vikwazo.
Benki ya Dunia ilikubaliana na hoja za Kiongozi wa Chama na kusitisha ufadhili huo mpaka pale Serikali ilipobadilisha sera na msimamo ili kuondoa ubaguzi na vikwazo kwa watoto wote wa kike kupata elimu pasipo kujali hali zao. Huu ulikuwa ushindi mkubwa kwetu kama Chama na kama nchi katika kutetea na kulinda haki za mtoto wa kike. Mpaka sasa tunafurahi kuwa watoto wote wa kike nchini wanapata fursa na haki ya elimu katika mfumo rasmi pasipo kubaguliwa kwa namna yoyote.
ACT Wazalendo inaungana na kila nchi ambayo inaweka mikakati bora, sera nzuri na mipango thabiti yenye dhamira ya kukuza, kuendeleza na kustawisha haki ya mtoto wa kike duniani zikiwemo elimu, afya, kulindwa dhidi ya ndoa za utotoni na changamoto nyingine zinazowakabili watoto wetu.
Aidha, tunazitaka serikali mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kuendelea kuchukua hatua imara ikiwemo kuzitathimini sera, mipango na taratibu zote za kusimimamia haki za mtoto wa kike ili kuhakikisha zinakuwa bora na zenye maana kwa maslahi ya mtoto wa kike wa Tanzania na kokote duniani.
Tunazitaka na kuzihimiza taasisi za serikali, Asasi za Kiraia, wadau na wanaharakati wengine kuendelea kupigania kuondoa vikwazo dhidi ya mtoto wa kike ili kuhakikisha uwepo wa mfumo bora wa maisha na ustwi wa maisha yake.
October 12, 2022
Home
Unlabelled
SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: TUONDOE VIKWAZO KUHAKIKISHA HAKI NA USTAWI WAKE
SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: TUONDOE VIKWAZO KUHAKIKISHA HAKI NA USTAWI WAKE
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment