HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 02, 2022

TET YAKABIDHI NAKALA 4400 ZA VITABU KWA TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVE NA NAKALA 31,100 KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI




Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 1/10/2022 imekabidhi jumla ya nakala 4,400 za vitabu vya kidato cha Kwanza hadi cha Nne kwa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Mwanamke Intiative Foundation (MIF) na nakala 31, 100 za vitabu vya kidato cha Tano na Sita kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Katika halfa hiyo ya makibidhiano iliyofanyika katika Skuli ya Dkt. Hasnuu Makame iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Leila Mohamed Mussa  amewaasa Walimu na Wanafunzi wavitumie vyema vitabu hivyo katika kupata Elimu bora.

"Hakuna Elimu ya kuhadidhiwa, Elimu inapatikana kwa katika vitabu hivyo mkavitumie na kuvitunza  vitabu hivi ili mpate elimu bora kwa Taifa" Amesema Mhe.Leila.

Pia amewataka wazazi na wanafunzi kutumia simu zao kuingia katika aktaba mtandao ya TET kuweza kujipatia machapisho mbalimbali kwani maktaba hiyo ni bure.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt.Aneth Komba amesema TET imetoa jumla ya nakala 4400  za vitabu zenye thamani ya shilingi Ml.51 laki 3.5  kwa MIF kwa ajili ya wanafunzi wa Kidato cha kwanza hadi cha nne  na nakala 31,100 za vitabu vya kidato cha 5 na 6 zenye thamani ya shilingi Ml 329 kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Dkt.Komba ameishukuru MIF kwa kuja na wazo la kutokomeza zero Unguja na kusema kuwa ni wazi wazo hili linapaswa kuwa Tanzania nzima kwani bado shule nyingi hazifanyi vizuri.

Aidha amesema ,licha na kukabidhi nakala ngumu, wanafunzi na walimu bado wana fursa ya kusoma machapisho mbalimbali katika Maktaba mtandao ya TET.

Aidha amesema, TET ipo tayari kutoa mafunzo kwa walimu wa Mkoa wa Unguja  ili waweze kupata ujuzi wa kumuandaa mhitimu aweze kujiajiri au kuajiriwa.

Naye Mwenyekiti wa MIF Mhe.Wanu Hafidhi Amiri ameishukuru TET kwa kukabidhi vitabu ambavyo vitasambazwa katika skuli 33 za Mkoa wa Unguja kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Mhe.Wanu amesema MIF ilifanya tafiti mbalimbali ili kubaini changamoto zinazosababisha wanafunzi wa Mkoa wa Kusini Unguja kufeli, moja ya changamoto ni uhaba wa vitabu vya kujifunzia kwa wanafunzi hivyo MIF ilichukua jukumu la kuomba TET kuwapatia vitabu vya kiada kwa shule za sekondari ambavyo vitasaidia kupunguza sifuri (zero) kwa wanafunzi hao.

Ameeleza  kuwa malengo ya MIF ni  kusaidia wanafunzi wa Zanzibar  kufaulu kidato cha Nne na kuiindoa Zanzibar katika shule 10 za mwisho Kitaifa katika matokeo ya kidato cha Nne.

No comments:

Post a Comment

Pages