HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 20, 2022

Wanachama JOWUTA watakiwa kugombea uongozi, kulipa ada

.
Katibu Mkuu wa JOWUTA Selemani Msuya akifungua semina ya siku mbili, kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwa wanachama wa chama hicho, inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa IFJ Afrika Sokhna Dia Coly akizungumza na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo Tanzania (JOWUTA), ambao wanashiriki semina ya mabadiliko ya tabianchi jijini Dar es Salaam


Na Mwandishi Wetu

 

WANACHAMA wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika chama hicho huku wakisisitiziwa kulipa ada ili kuwa wagombea wenye sifa.

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa JOWUTA Selemani Msuya wakati akifungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi iliyoandaliwa na chama hicho chini ya ufadhili wa Shirikisho la Waandishi wa Habari Afrika (IFJ).

Msuya alisema ni muhimu kwa wanachama wa JOWUTA kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni wa mwezi Novemba huku akisisitiza ili kuweza kuwa mgombea mwenye sifa huna budi kulipa ada.

“Kila mwanachama hai ambaye atakuwa amelipa ada anayosifa ya kuwania uongozi,  niwaombe tujitokeze kwa wingi tarehe ya uchaguzi  itakayopagwa mwezi Novemba, ili kuweza kupata viongozi bora wataoendeleza malengo na mambo mazuri yaliyoanzishwa,” alisema Msuya na kuongeza

“JOWUTA ni taasisi iliyosajiliwa na Serikali kwa lengo la kusimamia na kushughulikia matatizo yote yanayowakumba waandishi wa habari hivyo kama viongozi tutaendelea kulisimamia jambo hilo na watakaochaguliwa watalifanyia kazi kwa nguvu zao zote suala hilo,”alisema Msuya

Hata hivyo Msuya aliwataka waandishi wa habari waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo kujifunza kwa kina kisha kuhabarisha watu juu ya masuala yote yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.

“Chama hiki kina wanachama wengi lakini kwa siku hizi mbili za mafunzo ni waandishi wachache wamepta bahati kuhudhuria hivyo niwaombe wale wote waliopata nafasi hiyo kujifunza kwa kina na kisha kwenda kuhabarisha  na kuelimisha umma yale yote waliojifunza,” alisema Msuya

Vilevile Msuya aliishukuru IFJ kwa kufadhili mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitano Tanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kundi hilo linapata mafunzo ya kutosha ya kuwajengea uwezo.

Naye Mwakilishi wa IFJ Afrika, SokhnaDia Coly alitoa wito kwa waandishi wa habari kuongeza ushirikiano ili kukuza taasisi yao

No comments:

Post a Comment

Pages