Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla
hajaondoka nchini Oktoba 23, 2022, kwenda Korea ya Kusini kwa ziara ya
kikazi. Kulia ni Mkewe Mary Majaliwa, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo, Heri James na wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam kabla hajaondoka nchini Oktoba 23, 2022, kwenda
Korea ya Kusini kwa ziara ya kikazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 23, 2022) kwenda Seoul,
Jamhuri ya Korea kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Akiwa Korea Kusini, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa Han Duck-soo. Pia anatarajiwa kushiriki kongamano la biashara na kukutana
na wamiliki wa makampuni makubwa na wenye viwanda. Vilevile, atakutana na
Watanzania waishio Korea Kusini.
Kupitia vikao hivyo, Tanzania inatarajiwa kuimarisha mahusiano na Korea
Kusini ambayo yamedumu kwa miaka 30. Vilevile, kukuza mahusiano ya kibiashara na
uwekezaji, kuangalia fursa za kukuza uchumi wa bluu, utalii, mahusiano ya anga
na ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na utamaduni.
No comments:
Post a Comment