HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2022

  Askofu Dk. Kameta: Viongozi wa  dini tufanye kazi yetu ipasavyo



Na Mwandishi Wetu, Kibaha

 

IMEELEZWA kwamba viongozi wa kiroho wakifanya kazi zao kwa ipasavyo, watasaidia kuleta mabadiliko mazuri ya kijamii katika nchi.

 

Hayo yamesemwa na Askofu Dk. Lawrence Kametta kutoka Kanisa la TAG Aman Christian Centre, kwenye mahafali ya 10 ya Chuo cha Biblia Zoe Institute of Apostolic and Testimony, kilichopo Mlandizi. Kibaha mkoani Pwani.

 

DK. Kameta ambaye ni mmoja wa wahitimu katika chuo hicho, ngazi ya Udokta, amesema kwamba, viongozi wa dini wanatakiwa kusimamia nafasi zao, ili kuisaidia nchi kuwa na raia wema.

 

Akizungumza kuhusu matukio ya ukatili na watu kujinyonga na mauaji, ambayo yanaendelea kutokea baadhi ya maeneo hapa nchini, amesema kuwa yanatokana na watu kukosa hofu ya Mungu.

 

Amesema katika kukomesha matukio hayo, inatakiwa viongozi wa dini, kuzidi kuyakemea mara kwa mara na hali hiyo itasaidia kutoweka kwa matukio hayo.

 

"Viongozi wa dini ni watu na mamlaka ya kiroho, tutumie mamlaka tulizopewa kwa kuyakemea matukio hayo, kwa kuongea na jamii ili kufanikisha kuyatokomeza matukio hayo," amesema.

 

Akizungumza kuhusu mwaka mpya wa 2023 amesema inatakiwa kuziba nyufa sehemu ambayo haijaenda vizuri kwa mwaka ambao unakaribia kuisha 2022.

 

Amesema mwaka 2023 watu wafanye kazi, pia wawe na mikakati ya kimaendeleo, kama mikakati haitakuwapo, jamii itakuwa inarudi nyuma kimaendeleo.

 

John Mwakilema, ambaye ni mkuu wa chuo hicho, amesema chuo  kimejipanga kutoa elimu iliyo sahihi kwa watumishi wa Mungu, ambayo itazaa watumishi walio sahihi.

 

Kwa mujibu wa mkuu wa chuo huyo, kati ya wahitimu 42 wahitimu watano, wamehitimu shahada ya udaktari.

 

No comments:

Post a Comment

Pages