Amezindua
jengo hilo leo (Jumamosi, Desemba 31, 2022) ambapo amesema mbali na
kuboresha utendaji wa polisi pia jengo hilo litawarahisisha upatikanaji
wa haki kwa wananchi na kuwapunguzia gharama za kutembelea umbali mrefu
kufuata huduma.
Kadhalika,
Mheshimiwa Waziri Mkuu amekabidhi pikipiki mbili kwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini kwa ajili ya kituo hicho pamoja
na kituo kidogo cha Ndagala. Ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya
shilingi milioni 190.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema ujenzi wa
kituo hicho umefikia asilimia 99 na kwamba katika mwaka ujao wa fedha
wizara inakusudia kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne za
awali za askari wa kituo hicho.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi ifanye maboresho ya makazi ya askari katika mkoa huo ili waweze
kuishi katika mazingira bora Zaidi yatakayowawezesha kutekeleza majuku
yao ipasavyo.
Wakati huo
huo, Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) amekabidhi pikipiki 25 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Ruangwa ili ziweze kuwasaidia makatibu wa kata katika kufuatilia
utekelezaji wa Ilani.
No comments:
Post a Comment