HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 19, 2023

 Aga Khan Tanzania na Elekta Wasaini Mkataba wa Manunuzi na Uwekaji Vifaa Tiba vya Mionzi 

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Kwa kuzingatia maono ya Mtukufu Aga Khan, ya kuwezesha huduma bora za afya kupatikana kirahisi, Taasisi ya Utoaji Huduma za Afya ya Aga Khan, Tanzania (AKHST) kupitia Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCCP) imenunua moja ya kifaa cha kisasa cha tiba ya mionzi na vifaa vingine vinavyohusisha matibabu hayo vitakavyofungwa katika Kituo cha Huduma za Saratani cha Aga Khan kilichopo Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam (AKHD).

 

Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam itakuwa hospitali ya kwanza nchini Tanzania, na ya pili Afrika Mashariki na Kati kuwa na vifaa vya teknolojia hiyo.

Kwamba hii ineonesha kuwepo kwa maono na uvumbuzi unaolenga kusaidia wagonjwa ambapo leo imeshuhudiwa utoaji huduma bora za afya nchini na pengine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ukipata teknolojia bora zaidi ya matibabu ya saratani, na kuifanya kuwa kituo mahususi cha matibabu ya saratani Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa manunuzi wa vifaa hivyo jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam na Meneja wa Mradi Mtambuka wa Saratani Tanzania (TCC) Dkt. Harrison Chuwa amesema kifaa kitakachofungwa ni modeli mbili za linear accelerator kuongeza kasi ya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi.

Dkt. Chuwa ameongeza kuwa “Kusainiwa kwa mkataba huu manunuzi na uwekaji wa mashine ya mionzi unakifanya kituo cha matubabu ya saratani kuwa na mashine za kisasa, ya kwanza na ya aina yake nchini na Kanda ya Afrika Mashariki, ikiwezeshwa na CT simulator: Discovery TM RT kutoka kampuni ya GE Healthcare na Wide-bore, teknolojia ya MaxFOV inayoruhusu mwonekano kamili na sahihi, kingo-kwa-kingo, picha ya CT na teknolojia ya MicroVoxel ambayo hutoa na kutupatia miundo midogo, kuwezesha njia sahihi na kutoa DRR zenye mwonekano bora na usahihi wa picha,”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba na Afya, Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Dkt. Gijs Walvaren, amesema “ Lengo letu linabakia katika kukuza ubora wa utoaji wa huduma za afya na usalama wa wagonjwa na kuongezeka kwa upatikanaji kutoka huduma ya msingi hadi ngazi ya tatu/ juu kupitia uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikijumuisha vifaa, teknolojia, wafanyakazi waliofunzwa vyema na wenye uwezo pamoja na ithibati ya JCI ikifuatiwa na uidhinishaji ujao wa OECI, hizi zifuatazo kituo cha huduma ya saratani cha Aga Khan (AK-CC) kuwa moja ya vituo vya juu vya saratani barani Afrika na ulimwenguni,”.

Ameongeza “Pili, kituo hicho kitasaidia juhudi za Serikali katika kupanua huduma za matibabu ya saratani kwa Watanzania na kuongeza utalii wa kimatibabu katika ukanza mzima,”.

Nae, Makamu wa Rais, Huduma za Kimabara kutoka Elekta Feres Al Hasan amesema Kampuni ya Elekta ina kusudi moja ambalo linawapatia motisha kama kampuni na mtu binafsi.

“Matumaini kwa kila mtu anayehusika au kuguswa na Saratani. Hili linatuongoza kuelekea maono yetu ya kuwa ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kupata huduma bora ya matibabu ya saratani. Na tunapanga kufika huko kupitia dhamira yetu ya kuboresha maisha ya wagonjwa kwa kufanya kazi pamoja na wateja na washirika wetu,” amesema Al Hasan.

Kwamba kama mvumbuzi mkuu wa tiba ya mionzi, kampuni ya Elekta imejitolea kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anapata huduma bora zaidi ya saratani kadri iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment

Pages