HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2023

Mabadiliko sheria za habari Zanzibar wadau watakiwa kuongeza juhudi kupigania mabadiliko


Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt. Mzuri Issa akizungumza na waadishi wa habari vyombo tofauti kutoka Unguja na Pemba wakati wa uwasilishaji wa ripoti maalumu iliogusia changamoto katika utekelezaji wa tasnia ya habari.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuendelea na mkutano huo.


Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kimesema licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa  na wadau wa habari katika kupigania  mabadiliko ya sheria mbalimbali bado kunaonekana kugumu.


Kauli hiyo imetolewa huko Tunguu Zanzibar nje kidogo ya mji wa Unguja na Maneja uchechemuzi Tamwa Zanzibar ambaye pia ni afisa mdhamini baraza la habari la Tanzania upande wa Zanzibar Shiffa Said Hassan wakati akizungumza na waandishi katika mkutano wa kuwasilisha ripoti ya sheria za habari Zanzibar zilizofanyiwa mapitio na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na Shirika la INTERNEWS Tanzania ambazo zinakinza uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kujieleza


“Sisi kama wadau tumeshatoa mapendekezo yetu ya kuhitaji mabadiliko ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya tume ya utangazaji ya Zanzibar namba 7 ya mwaka 1997 na tunaendelea kufanya ushawishi ili tuweze kupata sharia bora zitakazotoa nafasi kwa wandishi na vyombo vya habari kutekeleza majukumu yake kwa uhuru,” ’Shifaa Said Hassan,.


Mkurugenzi wa Chama hicho Zanzibar, Dkt. Mzuri Issa akifungua mkutano huo alisema kuna haja ya taasisi husika za mabadiliko ya sheria kuweka kipaumbele kufanyiwa marekebisho yanayoendana na matakwa ya wadau katika sheria za habari Zanzibar ili zitoe mazingira ya uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari katika kutekeleza majukumu yao.

 


Alisema uhuru wa habari ni nguzo muhimu inayoweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ukuzaji wa maendeleo kwenye taifa loloote Ulimwenguni hivyo inapotokea sheria ya tasnia hiyo kubanwa ni sawa na kuchelewesha maendeleo ambayo yanahitajika na kila mtu.

 

“Bila ya uhuru wa habari na kujieleza itakuwa ngumu nchi yoyote kupata maendeleo, hivyo wakati wa kuzifanyia mabadiliko Sheria za habari umefika ili na sisi  nchi yetu ipege hatua” alieleza Dr Mzuri

 

Akitolea mfano changamoto za sheria hiyo alisema ni pamoja na Sheria namba nane, (27) (i) ya Wakala wa Habari Magazeti na Vitabu ambacho kinaeleza afisa yoyote wa Jeshi la Polisi anaweza kuzuia au kukamata gazeti lolote lile lisichapishwe iwapo atashuku linakwenda kinyume jambo ambalo linakwenda kinyume na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa kujieleza.


 “Tuna kila sababu ya kuona kwamba Sheria zetu, Sera na matendo yaendane na mikataba ya kimataifa kuhusu uhuru wa habari ili iweze kuleta maslahi kwa makundi yote,” alieleza Dkt. Mzuri Issa.

 

Aliongeza “tumepitia sheria kumi za habari na katika kufanya mapitio hayo tunasukumwa zaidi na mambo matatu. kama Zanzibar na Tanzania tunapaswa kwendana na mikataba ya kimataifa.”

 

 Wakichangia katika mkutano huo baadhi ya wanahabari walisema kuwa ni muda sasa ya wanahabari kujifunga kibwebwe hadi sheria ambazo haziendani na wakati ziondolewe.

“Lazima tupambane ili sheria zifanyikiwe kwani bila sheria hizo kubadilishwa hakuna heshima kwa waandishi wa habari hapa nchini” alisema Mwandishi Msomi Jabir Idirsa.

No comments:

Post a Comment

Pages