HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 19, 2023

 VIONGOZI WA SHIRIKA LA UNTOLD FOUNDATION WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

Na Mwandishi Wetu

Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Kimepokea wageni zaidi ya 300 ambao ni viongozi wa Shirika lisilo la kiserikali la Untold Foundation kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki. Imekuwa ni utaratibu wao wa kutembelea nchi mbalimbali ambazo Shirika hilo lina matawi yake na awamu hii ilikuwa Tanzania.

Vingozi wao waliweza kuandaa Safari ikiwa ni kutembelea vituo vya utalii vinavyopatikana Dar Es Salaam na moja ya kituo walichotembelea ilikuwa ni Makumbusho ya Taifa la Tanzania, kwenye kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Naye Mratibu wa safari hiyo ndugu Donald Mbeke alisema " tuliona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi kuwaleta wageni wetu ili waweze kujifunza juu ya Masuala ya uongozi, historia ya nchi yetu na utamaduni wetu". Aliendelea kwa kusema ni muda sana sijafika hapa Makumbusho ya Taifa nimekuta mambo yamebadilika sana. Alimalizia kwa kutoa shukrani kwa uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa ujumla namna walivyo waliwapokea na kuwapatia huduma rafiki kwa kila mmoja na kuahidi kurudi kwa awamu ya pili.

Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi alimshukuru Mratibu wa safari hiyo kwa kuona Makumbusho ya Taifa ni sehemu sahihi ya kutembelea na kujifunza, na kutoa wito kwa Mashirika mengine ya kiserikali na yasio ya Kiserikali pia kuiga mfano wa Shirika hili la Untold Foundation.


Makumbusho ni sehem sahihi sana kwa kujifunza historia ya nchi lakini zipo kumbi ambao wanaweza kufanyia Mikutano yao mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Pages