HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 12, 2023

TAKUKURU KYERWA YATAMBULISHA NA KUKABIDHI PROGRAM MPYA YA KUZUIA VITENDO VYA RUSHWA KABLA HAVIJATOKEA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bahati Henerco akizungumza baada ya kukabidhiwa Program ya TAKUKURU.

 

Na Lydia Lugakila Kyerwa

Taasisi ya Kuzuia  na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kyerwa mkoani Kagera imekabidhi na kutambulisha Program Mpya kwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo huku lengo likiwa ni Kuzuia vitendo vya Rushwa kabla havijatokea.

Akizungumza katika Kikao Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mpango wa Bajeti wa Mwaka 2023/2024  Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Kyerwa  Wilson Mwapwele amesema awali walienda katika mapambano zaidi ya vitendo vya Rushwa lakini kwa Sasa watajikita zaidi Kuzuia vitendo vya Rushwa kabla havijatokea  kwa kuanzisha Program hiyo iliyotajwa kwa jina la TAKUKURU RAFIKI.

Mwapwele amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 sura ya sita  inatambua kuwa Rushwa ni Adui wa Haki na kuwa Chama hakitavumilia vitendo vya Rushwa na ufisadi kwa namna yoyote ile.

"Mhe, Mwenyekiti Chama kimeelekeza Serikali kwa maana ya TAKUKURU pamoja na mambo mengine kubuni na kutekeleza Mikakati mipya ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi " alisema Mkuu huyo wa TAKUKURU.

Amesema pia Serikali imeelekeza kuhamasisha na kushirikisha Jamii katika Mapambano dhidi ya Rushwa.

Ameongeza kuwa kwa Mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 TAKUKURU ndiyo imepewa dhana ya kuongoza mapambano hayo ya Rushwa Nchini.

Mwapwele amesema Mapambano hayo yanalenga kuondoa Rushwa ambapo Program hiyo imebuniwa na Taasisi hiyo na itasaidia kujenga ukaribu na urafiki wenye tija na wadau na imewekwa kwenye Mpango mkakati wa TAKUKURU ambao umeanza kutumika mwaka 2020/2023 na unaotarajiwa kuisha mwaka 2025/2026.

Amesema Program hiyo imekusudia kuongeza wigo kwa ushiriki wa wadau katika kutambua na kutatua kero mbali mbali katika utoaji wa huduma za jamii na utekelezaji wa Miradi  mbali mbali ya Maendeleo.

Akizungumza baada ya kupokea Program hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ameoimba TAKUKURU kuendeleza Mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa bila kukata tamaa.

 "Program hiyo itahusisha jitihada za kutambua na kutatua kero za Wananchi zinazoweza kusababisha uwepo wa vitendo vya Rushwa katika Sekta mbali mbali za umma zikiwemo Sekta ya Afya, Elimu, Ardhi, Nishati, Barabara na Miradi mingine ambayo kwa kiasi kikubwa  inayotumia inatumia fedha nyingi za Serikali" alisema Kiongozi huyo.

Aidha, Program hiyo itaanza kutelezwa kuanzia Ngazi ya Kata kwa usimamizi na uratibu na Ofisi ya TAKUKURU na inategemea sana ushirikiano utakaojengwa katika Misingi ya Kuaminiana, kushirikiana, kuheshimiana kwa Watu wote.

 Amewahimiza Madiwani Wilayani Kyerwa kuvaa majukumu  ya kutatua Kero hizo kwa kushirikiana na Maafisa Watendaji wa Kata.

Hata hivyo Ameongeza kuwa kuna Makundi mbali mbali yanayotegemewa kuwa ni viongozi wa Vyama na Serikali, Viongozi wa Dini, Wana habari, Madreva Wanafunzi, Vijana wa Skauti, Watendaji mbali mbali wanaosimamia Miradi ya Maendeleo pamoja na Wazabuni.

Program hiyo imebeba Kauli Mbiu isemayo: KUZUIA* RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU TUTIMIZE WAJIBU WETU*

No comments:

Post a Comment

Pages