HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2023

Tamwa yatetea kuwepo sheria rafiki za habari

CHAMA cha Wandishi wa Habari Wanawake Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Internews Tanzania wamesema ipo haja kwa wandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko bora ya sheria za habari ambazo baadhi ya vifungu vyake vina changamoto katika sekta ya habari na wandishi wa habari.

 

Akizungumza na wandishi wa habari Tunguu Wilaya ya Kati Unguja, Mkurugenzi wa chama hicho, Dk. Mzuri Issa alisema vifungu hivyo vipo katika sheria ya Wakala wa Usajili wa Habari, Magazeti na Vitabu ya Na. 5 ya  mwaka 1988.

 

Alisema moja ya kifungu hicho ni kifungu cha 27(1) kinachoeleza Afisa polisi yeyote anaweza kukamata gazeti lolote pahala popote linapopatikana ambalo limechapishwa au ambalo anashuku kuwa limechapishwa kinyume na sheria hii, alisema kifungu hicho kinakandamiza sekta ya habari na vyombo vya habari.

 

Aidha alifahamisha kuwa waandishi wanapaswa kufanya jitihada zaidi ili kuhakikisha sheria na baadhi ya vigungu vinafanyiwa marekebisho au uondolewa kabisa.

 

Aidha alifahamisha kuwa wandishi wanapaswa kufanya jitihada zaidi ili kuhakikisha sheria na baadhi ya vigungu vinafanyiwa marekebisho au uondolewa kabisa.

 

“Ingawa sheria hii ilifanyiwa marekebisho lakini haikidhi haja kulingana na mazingira ya sasa ya utendaji wa sekta ya habari kwa kuzingatia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ili kuonesha msisitizo wa umuhimu wa kuwepo kwa sheria rafiki ambazo zitaenda sambamba na wakati,” alisema.

 

Jabir Idrissa, mwandishi wa habari mkongwe kwa upande wake alisema sheria inaathiri na kutishia utendaji wa wa kazi kwa waandishi wa habari.

 

Mtetezi wa haki za binadamu kutoka tasisi ya THRDC Zanzibar Shadida Ali, alisema sheria rafiki ni ile inayotoa uhuru mpana kwa kazi ya kukusanya, kuchakata na kutoa tarifa kwa umma sambamba na kurahisisha usajili wa vyombo vya habari ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi zaid.

 

Alisema ni vyema kwa taasisi husika kufanya marekebisho ya sheria hiyo kwa baadhi ya vifungu ambavyo ni kandamizi kutaleta uwajibikaji mzuri katika utendaji wa kazi za taasisi mbali mbali.

 

Nao baadhi ya wadau wa sekta ya habari Zanzibar walisema kifungu hicho cha sheria kwa kiasi kikubwa kinapelekea kusinyaa kwa uhuru wa habari.

 

Walisema kifungu hicho kikiendelea kutumika katika sheria hiyo basi itakuwa uhuru wa habari umeingiliwa na mamlaka mengine.

 

Mratibu wa kituo cha huduma na sheria tawi Pemba, Safia Saleh Sultan, alisema sheria hiyo ni ya zamani ambavyo sheria hiyo haiendani na mazingira ya sasa hivyo mamlaka ya polisi ni makubwa katika kuingilia sekta ya habari,

 

Alisema sekta ya habari kinaathirika na kifungu hicho jambo ambalo linawapelekea kufanya kazi kwa hofu    katika kufikisha tarifa kwa umma.

 

No comments:

Post a Comment

Pages