Mkuu wa Idara ya Kadi Benki
ya NMB, Philbert Casmir (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege
mmoja wa washindi wa safari ya kwenda Dubai wa Kampeni ya NMB Mastabata Kote
Kote, Upendo Msanjila, wakati wa wa hafla ya kuwaaga washindi saba na wenza wao
iliyofanyika leo Februari 27, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara
Benki ya NMB, Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum, Getrude Mallya (wa
pili kulia) na kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi, David Gusa. (NA
MPIGA PICHA WETU).
Mkuu wa Idara ya Kadi Benki
ya NMB, Philbert Casmir (wa pili kushoto) akimkabidhi mfano wa tiketi ya ndege
mmoja wa washindi wa safari ya kwenda Dubai wa Kampeni ya NMB Mastabata Kote
Kote, Edwin Mwakabage, wakati wa wa hafla ya kuwaaga washindi saba na wenza wao
iliyofanyika leo Februari 27, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara
Benki ya NMB, Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum, Getrude Mallya (wa
pili kulia) na kushoto ni Meneja Mwandamizi Idara ya Kadi, David Gusa. (NA
MPIGA PICHA WETU).
Mkuu wa Idara ya Kadi Benki
ya NMB, Philbert Casmir (kushoto) akimkabidhi tiketi ya ndege mmoja wa
washindi wa safari ya kwenda Dubai wa Kampeni ya NMB Mastabata Kote Kote, Rose
Qamara wakati wa hafla ya kuwaaga washindi saba na wenza wao iliyofanyika leo Februari 27, 2023 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara Benki ya NMB,
Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum, Getrude Mallya (wa pili kulia).
NA MWANDISHI WETU
WASHINDI
7 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya kadi iliyoondeshwa na Benki ya
NMB 'NMB MastaBata - Kote Kote' wameagwa na kukabidhiwa tiketi za safari
yao ya Dubai iliyolipiwa gharama zote, na tayari wamendoka nchini leo
mchana.
Hafla
ya makabidhiano na kuwaaga washindi hao na wenza wao, imefanyika Makao
Makuu ya NMB, ambapo walikabidhiwa tiketi zao na Mkuu wa Idara ya Kadi
ya NMB, Philbert Casmir.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Casmir alisema kwamba malengo matatu ya kampeni
hiyo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akiyataja kuwa ni pamoja na
kuhamasisha matumizi ya kadi, ambayo ni rahisi, nafuu na salama zaidi,
kuliko matumizi ya pesa taslimu, ambayo ni hatarishi na ya gharama
kubwa.
"Malengo
mengine ya NMB MastaBata yalikuwa ni kurejesha kwa wateja sehemu ya
faida jambo linalothibitisha namna tunavyowajali, lakini pia kampeni
ililenga kuthibitisha uimara wetu katika masuluhisho ya kidijitali,
ambako NMB tumefanya uwekezaji mkubwa.
"Katika
hili, NMB tumeshirikiana na MasterCard na tunawatakia washindi wetu
ambao wataongozana na maafisa wa benki yetu safari njema, ambayo
tunaamini itakuwa na siku nne zenye mambo mengi ya kujifunza, ikiwemo
fursa za kibiashara na utalii," alisema Casmir.
Aliongeza
ya kwamba, mwisho wa NMB MastaBata 'Kote Kote' iliyoanza Oktoba 28
mwaka jana, ni mwanzo wa kampeni nyingine mbalimbali, huku akiwataka
Watanzania na wateja wa NMB kukaa mkao wa kuchangamkia kila fursa
inayokuja kupitia huduma za benki hiyo.
Washindi
na wafanyakazi wawili waliokabidhiwa tiketi na kuondoka jana mchana ni
pamoja na Rose Qamara, Upendo Msanjila, Edwin Mwakabage, Nazia Lakha,
Xaveria Hyera, Chintan Kamania na John Lubisha.
Akizungumza
kwa niaba washindi hao, Upendo Msanjila alikiri kufurahishwa sana na
safari hiyo, ambayo awali wakati akipigiwa simu ya ushindi hakuamini
akihisi ni matapeli na kwamba NMB imewezesha kwa mara ya kwanza yeye
kutembelea Dubai akiwa na mwenza wake.
Naye
John Lubisha, alielezea kiwango cha juu cha furaha yake kwa kushinda
moja kati ya nafasi saba zilizokuwa zikishindaniwa na wateja zaidi ya
Milioni 5 benki hiyo katika kipindi cha miezi mitatu iliyojumuisha
zawadi zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350.
No comments:
Post a Comment