HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2023

TCU Serikali imetenga bilioni 6.4 Kwa ajili ya kuimarisha uthibiti na ubora wa mitaala.


Na Jasmine Shamwepu, Dodoma 


Katibu Mtendaji TCU Prof. Kihampa amesema kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 6.4 kupitia Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi kwaajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo vikuu iko katika hatua mbalimbali zakufanyiwa mapitio.



Aidha, Prof. Kihampa amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba, 2022, jumla ya viongozi na wanataaluma 575 wameshanufaika na mafunzo hayo ambayo yamelipiwa na Serikali kwa asilimia 100. Kutokana na hatua hizi zinazochukuliwa na Serikali, vyuo vikuu vimeweza kuimarisha mifumo yake ya uthibithi ubora na uendeshaji wa mafunzo.


Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof.Charles  Kihampa leo wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume hiyo kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.


 Amesema kuwa TCU imeweka utaratibu wa kuanzishwa na kuimarishwa mifumo ya uthibiti ubora ndani ya vyuo vikuu ambapo vyuo vyenyewe vimekuwa na utaratibu wa kujikagua,kujitathmini na kufanya marekebisho mbalimbali kwa kuzingatia miongozo ya uendeshaji wa vyuo vikuu. 


Katika hatua nyingine tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU imewataka  wanafunzi kutoka Tanzania wanaosoma kwenye nchi zenye changamoto za kiusalama ,kurudi nchini nakufanya utaratibu uliwekwa ili waweze kujiunga na vyuo vikuu nchini na kiendelea na masomo yao.


Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tume hiyo inawasaidiaje wanafunzi wanaosoma kwenye nchi zenye machafuko kama Urusi na Ukrain ,ikiwa ni siku chache kupita Mtanzania aliyeenda kusoma Ukraine kufariki baada ya kupigwa risasi.


Ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuongezeka kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini ambapo Serikali imeendelea kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kuongeza wigo wa fursa za masomo ya elimu ya juu kwa watanzania.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotokewa na  Prof.Kihampa amesema Tanzania imeendelea kuwa Taifa la watu wenye maarifa ,ujuzi,weledi na uwezo wa kutatua changamoto za kijamii na uchumi kwa manufaa ya wananchi wake ifikapo mwaka 2025 pamoja na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati unaochochewa na uwepo wa viwanda.


Idadi ya Wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 259,266 mwaka 2020/21 hadi 295,919 mwaka 2021/22 sawa na asilimia 14.1. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka kwa mwaka wa masomo 2022/2023.

No comments:

Post a Comment

Pages