HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 23, 2023

WANANCHI WATAKATA WAKIKWEA PIPA KUWAFUATA REAL BAMAKO

 

Na John Richard Marwa


Klabu ya Yanga imekwea pipa usiku wa kuamkia leo kuwafuata Real Bamako ya Mali katika ngalambe za Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC mchezo utakaopigwa February 26.


Wakati Yanga wakiondoka kuelekea Mali, safari yao imechagizwa na ushidi wa bao moja mtungi dhidi ya KMC FC mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NBC PL na kuelekea kujikita kileleni mwa msimamo wakifikisha pointi 62 michezo 23 huku watani zao Simba SC wakisalia nafasi ya pili na pointi zao 54 wakiwa na michezo sawa huku kila mmoja akisaliwa na mechi saba.


Ushindi huo kwa Yanga ni wa 10 mtawalia tangu walipopoteza dhidi ya Ihefu FC huku wakipata 'clean sheet' 9 wakikusanya pointi 30.


Haukuwa mchezo wa kuvutia kwa namna ambavyo watu wengi walitegemea, Yanga licha ya kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi bado KMC walishindwa kufanya chochote kwenye mchezo huo na kuonyesha mpira mbovu.


KMC wanasalia nafasi ya 12 kwenye msimamo wa NBC PL na pointi zao 23 michezo 23 wastani wa pointi moja kila mchezo.


No comments:

Post a Comment

Pages