Na Mwandishi Wetu
Makombe yaanza kurejea nyumabani Manchester United. Ndivyo unaweza kuelezea mara baada ya Mashetani Wekundu kutwaa taji la Carabao Cup hapo jana ikiwa ni miaka sita bila ya kunyanyua makwapa.
Manchester United chini ya Kocha Erick Ten Hag jana ilitwaa taji hilo kwa kutoa adhabu kali kwa vijana wa Newcastle United ya mabao (2-0) katika Dimba la Wembley.
Fainali kwa ajili ya kushinda, Man United walizuia vizuri sana , ndani ya Boksi wamedili na kila mpira ambao Newcastle walijaribu kupeleka , nje penati Boksi , United walikuwa !wanafunga nafasi haraka sana yasipigwe mashuti na pasi za ndani kwenda nyuma yao , pembeni ya uwanja mabeki wa pembeni wa United walipata msaada haraka kutoka kwa viungo wao . Ndio maana Newcastle walipata shida kutengeneza nafasi nzuri za kufunga
Newcastle walikuwa wanatia presha vizuri sana hasa eneo la kiungo , nia yao kubwa ni kuwanyima nafasi Casemiro na Fred kupiga ile pasi ya kwanza ya kuanzisha shambulizi la kushitukiza , waliwalazimisha kwa muda mrefu United kutumia mipira mirefu wakijua wataokota mipira ya pili inayodondoka.
Man United wana wachezaji kadhaa wazuri wakiwa na mpira mguuni , na wakiwa wafanisi , wanakupa shida : wana wachezaji ambao wapo tayari kufanya mikimbio nyuma ya safu yako ya ulinzi ( Vertical runners ) , na kama Man United wangekuwa makini basi Newcastle wangefungwa zaidi ya magoli mawili
Newcastle mapishi yao ya mabeki watatu nyuma ( Schar Botman na Burn ) Trippier anasogea juu zaidi kumruhusu Almiron kupokea mpira akiwa ndani wakati Saint Maximin anatakiwa kutanua zaidi uwanja ( 3-2-2-3 ) lakini kwasababu Man United waliamua kuzuia kwa 4-5-1 maana yake waligoma kuzidiwa idadi ya wachezaji pembeni ya uwanja na katikati ya uwanja
No comments:
Post a Comment