HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 12, 2023

Balozi wa Marekani Mgeni rasmi Hafla ya Kifungua Kinywa kwa Wanawake


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Michael Battle anatarajia kuwa Mgeni rasmi katika Hafla ya Kifungua Kinywa kwa Wanawake( Accelerates Executive Women's Breakfast) itakayofanyika Machi 18 mwaka huu katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini humo Mkurugenzi wa Kampuni ya Accelerate Business Group Bernice  Fernandes amesema kuwa lengo la hafal hiyo katika kuwaezesha wanawake ni kutoa fursa kwa watendaji, wajasiriamali na viongozi wenye mawazo ya kitalaam kwa mtandao wa kubadilishana mawazo juu ya uwezeshaji wa wanawake.
 

Ameyataja malengo mengine ni wanawake kujifunza kutoka kwa viongozi wazoefu waliofanikiwa, kujadili mikakati ya kuvunja vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya wanawake na kutambua fursa za kusaidia mipango ya kuwezesha.

" Tunafurahi kuwashikilia wanawake hawa mashuhuri amabao wamevunja dari katika kazi zao. kama mwanamke ni muhimu kuungana na kushirikiana katika mafanikio tuliyoyapata. Pia inatia moyo kusikia safari za wanawake hawa katika nafasi zao za uongozi," amesema Bernice.

Amesisitiza kuwa hafla hiyo itatoa ufahamau na msukumo mkubwa kwa washiriki wote katika kuchangia sababu za uwezeshaji wa wanawake katika jamii kufikia malengo ambayo wanayatamani.

Kwa upande wake, Mjumbe Mtenfdaji wa Kampuni hiyo, Teddy Chamshama, amewahimiza wanawake kushiri hafla hiyo ikatayoanza kuanzia Saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana kwani watapata fursa ya kubadilshana mawazo na wanawake watendaji wa makampuni waliofanikiwa.

Chamshana amefafanua kuwa wanawake wanaohitaji kuhudhuria hafla hiyo wanatakiwa kufuatilia kurasa za mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo na kupiga simu 0692818823 ili kujua utaratibu wa kupata tiketi au kufika hotelini hapo.

Nae, Muuguzi kutoka Premier Care ambao ni sehemu ya wadhamini, Emma Kamande amesema siku hiyo watatoa huduma za afya bila malipo na kwamba wanawake watakaohudhuria watafanyiwa vipimo vya magonjwa ya presha, sukari pamoja na upimaji uzito. 


No comments:

Post a Comment

Pages