HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 12, 2023

Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope yatoa Msaada wa Mafuta kwa Wanafunzi Wenye Ulemavu wa Ngozi

Na Hussein Ndubikile, Dar  es Salaam 


Taasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) imetoa msaada wa mafuta ya ngozi kwa wanafunzi Wenye Ulemavu wa Ngozi huku ikibainisha kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazozifanya za kusaidia watu wenye ulemavu na shughuli za miradi ya maendeleo.
Akizungumza katika hafla ya utoaji wa msaada iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Michael Salali amesema kuwa wamekuwa wakijihusisha katika utoaji misaada kwa makundi maalum na kwamba anaamini mafuta hayo yatawasaidia wanafunzi kuwakinga na mionzi ya jua.

" Tumeshatoa misaada kwa makundi ya watu wenye ulemavu tunatoa mafuta haya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia tunaomba wadau watuunge mkono," amesema Salali.

Amebainisha kuwa kabla ya kutoa msaada huo tayari walishatoa Bima kwa Watu 1,000 na vifaa vingine vya kuwasaidia watu wenye ulemavu hivyo wataendelea kushirikiana na Serikali kusaidia makundi maalum.

Akimpongeza Rais Dkt. Samia amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi amefanya mambo ikiwemo kuboresha miundo ya afya, elimu na usafirishaji na kwamba ameonesha kuwajali walemavu.

Kwa upande wake, Naibu Spika ambaye pia na Mbunge wa Jimbo la Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada iliyoutoa kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi na kuziomba taasisi zingine kuiga mfano.

Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ameipongeza FDH kwa jinsi inavyowajali watoto wenye ulemavu na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia.

Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mwalimu Beatrice Edward ameipongeza taasisi hiyo inavyojitoa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu huku akiziomba taasisi kujitokeza kusaidia watoto wenye mahitaji maalum.


No comments:

Post a Comment

Pages