HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2023

Bilioni 44.6 mfuko wa fidia Kwa wafanyakazi (WCF)umelipa mafao kwa wanufaika


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Machi 02, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma.



Na Jasmine Shamwepu, Dodoma




Jumla ya Shilingi Bilioni 44.61 mfuko wa fidia Kwa wafanyakazi (WCF) umelipa mafao  kwa wanufaika mbalimbali ikiwa ni ongezeko kubwa kwa kulinganisha na kipindikabla ya kuanza kwa WCF ambapo malipo ya fidia yalikuwa chini ya Shilingi Milioni 200 kwa mwaka.


Katika kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022, WCF ililipa mafao ya jumla ya Shilingi Bilioni 6.19 kwa wanufaika 1,004 na hivyo kufanya wanufaika wa Mfuko toka kuanzishwa kwake kufikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya Shilingi Bilioni 49.44.  


Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma amebainisha hayo wakati wa akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari.


Dkt Mduma amesema mfuko huo umeendelea kulipa fidia hizo kupambana na umaskini na kufanya malipo endelevu (pensheni) kwa wanufaika ambapo kwa mwezi Juni 2022, wanufaika 1,114 walilipwa kiasi cha Shilingi Milioni 231.39 kwa mwezi huo.


Katika hatua nyingine, Dkt. Mduma amesema kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2021 hadi Februari 2023 Waajiri wapya 5,250 wamejisajili WCF huku kati ya waajiri hao asilimia 99.27% ni waajiri wakubwa ,huku asilimia 98.71% ni waajiri wa kati na waajiri wa chini ni asilimia 88.56%.


Mfuko huu umekuwa na faida kubwa kwani lengo,lake kubwa ni kuwakomboa wafnykazi waliopata madhili ama majanga wakiwa kazini kutoka katika dimbwi la umasikini ambapo takwimu za hivi karibuni zikionesha tangu kuanzishwa, idadi ya wanufaika wa Mfuko imefikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya shilingi Billioni 49.44,"amesema Dkt. Mduma.


Aidha amesema waajiri wengi kwa sasa wanavutiwa kujisajili na WCF kutokana na Serikali sikivu ya awamu ya sita kupunguza kiwango cha mchango kwa sekta binafsi kutoka asilimia 1 ya hapo awali kabla ya maboresho ya kisera hadi asilimia 0.5 ya sasa hivyo kuleta mlingano wa michango kuwa sawa na sekta za umma.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeendelea kuboresha, kuhakikisha huduma muhimu kwa wadau nchi nzima kwa njia ya mtandao kufikia malengo ya Mfuko huo.

No comments:

Post a Comment

Pages