HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 27, 2023

KATIBU MSAIDIZI DAA ABWAGA MANYANGA



Flex Chunga (kulia), akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa RT Kanda ya Pwani, Novemba mwaka jana jijini Dodoma.


Chunga, akiapa mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe Kamati Tendaji RT, Novemba mwaka jana.


NA MWANDISHI WETU


KATIBU Msaidizi wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Felex Chunga, ametangaza kujizulu nafasi hiyo kuanzia Machi 26, mwaka huu.

Chunga, amefikia uamuzi huo kutokana na kubanwa na matakwa ya kikanuni ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambapo kiongozi mmoja hapaswi kuwa na nyadhifa mbili kwa wakati mmoja katika mchezo mmoja.

Mbali na kuwa Katibu Msaidizi DAA, Chunga pia ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Kanda ya Pwani.

Kutokana na matakwa hayo ya kikanuni, Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Wakili Msomi Jackson Ndaweka, aliwaandikia barua viongozi watatu wa shirikisho hilo ambao wana nyadhifa zaidi ya moja, kuwataka kutekeleza takwa hilo.

Viongozi hao mbali na Chunga, ni pamoja na Amon Mkoga Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kanda ya Magharibi na Lwiza John Katibu wa Riadha Mkoa wa Mbeya na Mjumbe Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 27, Chunga alisema tayari amewasilisha barua ya kujizulu nafasi ya Katibu Msaidizi DAA kuanzia Machi 26 na sasa atabaki kuwa Mjumbe wa RT Kanda ya Pwani, ikiwa ni katika kutekeleza takwa hilo la kikanuni.

Pia, Lwiza John naye tayari ameachia nafasi ya ukatibu Mkoa wa Mbeya, ambapo Mkoga bado hajatekeleza takwa hilo la kikanuni hadi sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages