HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 27, 2023

MAMA MARIA NYERERE APEWA TUZO YA HESHIMA YA MALKIA WA NGUVU 2023


 Na Khadija Kalili


MKE wa wa  aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere Mama Maria  Nyerere jana usiku ametunukiwa zawadi ya Malkia wa Nguvu  ya mwaka 2023  kwenye killele kilichofanyika kwenye ukumbiwa  Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.



Tuzo hiyo ya Heshima imetolewa na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson na  kumkabidhi Mkuu wa  Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ambaye  pia ni mtoto wa mama Maria Nyerere.


Tuzo hizo za Malkia wa Nguvu   zimefanyika  kwa mara ya saba  sasa zimeandaliwa na Clouds Media Group na kudhaminiwa na CRDB Bank  , Kilombero Sugar ' Bwana Sukari', Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), DSTV,Classic Finnishers.

Wanawake wengine walio pata tuzo kwenye vipengele mbalimbali.


Tuzo ya Uongozi imekwenda kwa Kamishna Generali wa Jeshi la  Uhamiaji Anna Makakala.


"Namshkuru mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa kuendelea kuniamini  pamoja na viongozi wote wa Wizara  ya Mambo ya Ndani  ya nchi kwa kumpa ushirikiano katika kazi zangu  za kila siku za kukitumikia taifa" amesema Kamishna Makakala.mara baada ya kupokea tuzo hiyo. Uhamiaji,  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanesco Somoe Ismail aliyepata Tuzo ya Funguo ya maisha  kusababisha kwa kuwashika mkono Malkia wengine katika eneo lake la kazi.


Tuzo ya  Ubunifu na uvumbuzi ilikwenda kwa Tasila Melita ambaye amebuni mashine ya kuteketeza taulo  za  kike  wanazotunia wanapokuwa kwenye hedhi, Tuzo ya Ustawi wa Jamii imenyakuliwa na Dkt.Stella Rwezahura ambaye ni Daktari bingwa wa damu ambaye ndiye alisimamia  upandikizwaji wa uloto kwa wagonjwa 11  wenye saratani ya damu nchini huku Tanzania ikiwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kutoa matibabu haya.


Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo yake Dkt.Rwezahura amesema kuwa  jamii inapaswa kuondokana na imani potofu kuwa ugonjwa huu ni wa kurogwa hivyo mara wanapogundulika wanatakiwa kwenda hospitalini mara moja kwa sababu unatibika ni wa kurithi kama ilivyo selimundu na upo duniani kote.


"Naishkuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kunipa nafasi  ya kusoma nakuwa Daktari bingwa  wa damu  kwani wakati naanza kusoma kukikua na madaktari bingwa wa damu  wawili tu na walikua wakikaribia kustaafujapo awali nilipenda kuwa daktari wa wanawake hivyo nilikubali ushauri niliopewa na kwa sasa nawajibika kwa ajili ya taifa langu najivunia hili na nawashukuru wote pamoja na familia yangu" amesema Dkt. Rwezahura.


Wengine waliopata tuzo ni  Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Foundatin Tuli Ester  Mwambapa  aliyepata tuzo ya mhamasishaji bora wa mwaka  .


Tuzo ya Malkia anayesabababisha ajira ilikwenda

 kwa  mmiliki wa Kampuni ya Zara Tours ambaye ametoa ajira kati ya  300 hadi 600 katika ya utalii nchini washindi wote wamepewa  tuzo  pamoja na hundi ya Mil.3 kila mmoja zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).


Usiku huo wa Malkia wa Nguvu  2023 umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Rais wa awamu ya nne Mama  Salma Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Sophia Mjema na wawakilishi kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini.

No comments:

Post a Comment

Pages