Mkurugenzi wa TWCC Mwanaidi hamza akizunguma na wajasiriamali hawapo pichani kwenye Ukumbi wa Mikutano Mlimani City Jijini Dares es Salaam.
Na Khadija Kalili
MAKAMU MWENYEKITI wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Victoria Mwanukuzi ametoa wito kwa watanzania wote kuthamini na kununua bidhaa za ndani kwani ndiyo njia kubwa ya kuweza kuzipandosha thamani na kukuza uchumi wa wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla.
Makamu Mwenyekiti Mwanukuzi amesema hayo leo Machi 10 alipokua mgeni rasmi alipozungumza kwenye kongamano la wajasiriamali na wafanyabiashara wanawake kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.
"Tumekutana leo ikiwa ni latika muendelezo wa kusherehekea siku ya Mwanamke Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi nane ambapo sisi tumeiita siku ya wajasiriamali wa Afrika bado tunaendelea kusherehekea pamoja hivyo nawasisitiza tupende kununua bidhaa za nyumbani kwa sababu zina ubora madhubuti kushinda hata hizo bidhaa za nje kwa sababu sisi bidhaa zetu ni za asili" amesema.
"Tuhamasishane kupenda vya nyumbani mimi binafsi nikiingia kufanya manunuzi kwenye maduka makubwa 'Super Market' huwa nanunua bidhaa zilizoandikwa Made in Tanzania yote hii ni kwa sababu ya kuwa na uzalendo" amesema Mwanukuzi.
Mhandisi Lightness Salema ambaye pia ni miongoni mwa wajasiriamali amesema kuwa wakati umefika kwa mjasiriamali ili anyanyukelazima ajinyanyue mwenyewe ndipo atainuliwa na kusogezwa huku akisisitiza lazima mwanamke awe mwaminifu kwenye biashara kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuweka taarifa za biashara zake.
Mkurugeni wa TWCC Mwajuma Hamza amesisitiza kuwa hivi sasa tunaelekea katika soko huru la Afrika hivyo wajasiriamali ni wajibu wao kujituma.na kujikuza ili kuweza kukabiliana na ushindani wa biashara wakati utakapo fika licha ya kuwa wanakabiana na changamoto mbalimbali.
No comments:
Post a Comment