Na Jasmine Shamwepu, Dodoma
JESHI la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kujiunga na jeshi hilo kwa vijana wa kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidato cha Nne hadi Shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa mafunzo ya kujitolea JKT na kurudishwa majumbani huku akitahadharisha jamii kuepuka matapeli.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano Luteni Kanali Gaudentius Ilonda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kupitia tangazo hilo watajitokeza matapeli wanaotaka kujipatia pesa kinyume na utaratibu.
"Matapeli wanapenda kutumia mwanya huu hivyo niitake jamii wazazi na walezi kutokubali mtu yoyote atakapo pigiwa simu au mtu yoyote kwamba ana nafasi hizo," alisema Luteni Kanali Ilonda.
Katika hatua nyingine ametaja sifa za muombaji ni lazima awe ni raia wa Tanzania,awe na umri kuanzia miaka 18 Hadi 26 Kwa wenye elimu ya kidato Cha Nne hadi Cha sita na umri usiozidi mika 27 Kwa wenye elimu ya juu,awe na afya nzuri na akili timamu,awe mtanzania mwenye tabia na nidhamu nzuri ambaye hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai, Mahakamani na kufungwa.
"Sifa ya muombaji nyingine awe na cheti halisi Cha kuzaliwa (Original birth certificate) vyeti vya shule na vyeti vya taaluma, awe hajatumikia jeshi la polisi,magereza, chuo Cha mafunzo au kikosi maalumu Cha kuzuia magendo,awe amehitimu mafunzo ya jeshi la kujenga taifa Kwa mkataba wa kujitolea miaka 2 na kutunikiwa cheti na asiwe ameoa au kuolewa," amesema
Aidha amesema utaratibu wa kutuma maombi ni pamoja na maombi yote yatumwe Kwa mkono na yawasilishwe makao makuu ya jeshi Dodoma kuanzia Leo tarehe 9 Hadi 20 March yakiwa na viamabatanisho nakala ya kitambulisho Cha taifa au namba ya NIDA,nakala ya cheti Cha kuzaliwa vyeti vya shule na chuo,nakala ya cheti Cha JKT na namba ya simu ya mkononi ya muombaji.
No comments:
Post a Comment