HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 01, 2023

MATUMIZI YASIYO SAHIHI YA VIUATILIFU YANAMUONGEZEA GHARAMA MKULIMA DK. NDUNGURU

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

MEELEZWA kuwa Matumizi yasiyosahihi  ya viutilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu na mazao ya mimea imekuwa kikwazo   katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa Mimea nchini.



Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi  Mkuu  wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania,(TPHPA) Dkt. Joseph Ndunguru  wakati akielezea  majukumu ya mamlaka hiyokatika kipindi Cha Serikali ya awamu ya sita.


Dkt. Ndunguru amesema kuwa  Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.

Aidha Dkt.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi  na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.

“Matumizi yasiyosahihi  ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea,”amesema Dkt.Ndunguru

Akitoa takwimu za Uchambuzi wa sampuli mbalimbali zilizofanywa na  Mamlaka hiyo ,Dkt.Ndunguru ameeleza kuwa sampuli 1025 za viuatilifu (analysis of pesticide samples) ambazo zimeshafanyika ikiwa sampuli 1005 sawa na asilimia (98.04%) zilikidhi viwango huku sampuli 20 (1.96%) zimeonesha kutokidhi viwango

Aidha Dkt.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima  kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi ,inaathiri afya yake na mazingira.

No comments:

Post a Comment

Pages