HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2023

TANZANIA YAFUZU PARAOLIMPIKI GHANA


Na Mwandishi Wetu


Timu Za Wanaume Za Mpira Wa Kikapu Wa Watu Wenye Ulemavu (wheelchair Basketball).

Zimefuzu kushiriki katika michezo ya Paralimpiki nchini Ghana mwezi Agosti.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka la Watu wenye ulemavu Tanzania (TWBA) imethibitisha.


"Timu ya Tanzania imefuzu kuwakilisha Kanda ya Mashariki pamoja na nchi ya Kenya baada ya nchi nyingine 8 kutotimiza vigezo Na Taratibu Za Ushiriki.


"Upande wa timu za wanawake bado kutakuwa na mchezo wa mtoano wa mikondo mitatu ya kumtafuta mshindi wa jumla kati ya Tanzania na Kenya na Mchezo huo umepangwa kufanyika mwanzoni mwa Mei na Tanzania tumepewa uenyeji wa michezo hii. Kuanzia tarehe 5 hadi 7 Mei jijini Dar es Salaam" imemaliza taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages