HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 09, 2023

MAYELE AONGOZA MAUAJI KWA AS BAMAKO

Na John Richard Marwa

Mshambuliaji kinara wa klabu ya Wananchi Fiston Mayele ameiongoza Young Africans kuiangamiza klabu ya AS Bamako ya Mali katika Dimba la Benjamin Mkapa jioni ya leo.

Mayele ambaye alifunga Bamako mchezo wa kwanza uliopigwa wikiendi iliyopita nchini Mali na kutoka sare ya bao moja kwa moja leo amefunga tena katika mchezo wa nne wa kundi D la Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAF CC msimu huu wa 2022/23.

Mayele aliingia kambani dakika ya nane ya mchezo akipokea pasi elekezi ya Kennedy Msonda baada ya safu ya ulinzi ya AS Bamako kufanya makosa wakiwa wanajenga shambulizi.

Bao la pili limewekwa kimiani na Jesus Moloko akimpokonya beki ambaye akishindwa kuuondosha mpira ambao ulikuwa kwenye eneo lao wakijenga shambulizi.

Licha ya ubora wa kikosi cha Kocha Mohamed Nabi kwenye mchezo wa leo Real Bamako wametoa mechi ngumu sana kwa Yanga hasa katika eneo la kiungo ambapo Yanga walipata tabu kuwazibiti.

Yanga kwa ushidi huo wamefikisha pointi saba na kusalia nafasi ya pili kwenye kundi D ambalo kinara ni  US Monastiry ambao wameichakaza TP Mazembe kwa bao moja kwa bila nankufikisha pointi 10 jioni ya leo.

Yanga watahitaji kushinda mechi inayofuata dhidi ya US Monastiry ambayo itapigwa Machi 19 Dimba la Benjamin Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Pages