HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2023

MZUMBE DAR YACHANGIA MATIBABU KWA WATOTO WALIOLAZWA MUHIMBILI


Mkuu wa Idara ya  Ustawi wa Jamii Bw. Daniel Mutani akiwashukuru wafanyakazi wa Ndaki ya dar es Salaam kwa mchango wa matibabu walioutoa ilikusaidia matibabu ya watoto.
 

Baadhi ya wafanyakazi wafanyakazi wa Chuo kikuu Mzumbe na maafisa kutoka hospotali ya Taifa Muhimbili katika Picha ya pamoja.

Kaimu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Coretha Komba akikabidhi mchango kwa Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Ester  Mwambogoja.

 

Na Mwandishi Wetu
 

Wanajumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya watoto na kutoa msaada kwa kuchangia matibabu yenye thamani ya Sh. Mil 1.5 kwa watoto  waliolazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofikia kilele tarehe 8 Machi 2023.


Akizungumza  kabla ya kukabidhi msaada huo leo tarehe 7 Machi 2023, Kaimu Mkuu wa Ndaki hiyo, Dkt. Coretha Komba anamshukuru Mungu ambaye ametujalia uzima  wanajumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe na kuweza kuja hapa ili tuweze kuwapa msaada wa matibabu watoto ambao wanauhitaji.   Tunawapongeza sana Kwa kazi mnayoifanya hapa. 


“Sisi tumekuja pia Ili tujifunze, kama kauli mbiu yetu inavyosema; 'Tujifunze Kwa Maendeleo Ya Watu'. tunaamini leo ni mwanzo wa kuendelea kushirikiana ili tuweze kuwasaidia hawa watoto kwa maendeleo yao na Taifa. Hivyo tutaendelea kuja na kutoa misaada pale inapohitajika”.Amesema Dkt. Komba.


Akipokea msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Ester Mwambogoja amewashukuru wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kuchangia matibabu  na  amewaomba wafanyakazi hao kutokuishia hapo.  Pia amewakaribisha kufika hospitalini kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali mara wapatapo nafasi kwani inawapa faraja.


Aidha, mmoja wa wahadhiri wa Chuo hicho, Dkt. Godbertha Kinyondo ameshauri Hospitali ya  Muhimbili kushirikiana na vyuo kikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe  kwani  wanachuo hasa wanaosomea Shahada ya uzamili (Masters) hufanya tafiti zinazolenga kuangalia changamoto mbalimbali. Hivyo, hospitali inaweza kushirikiana na Chuo ili kuweza kupata mada za kufanya utafiti zinazohusiana na aina fulani ya magonjwa na mazingira wanayotoka wagonjwa na kufanya utafiti utakaotoa majibu na mbinu za kipambana na magonjwa hayo.


Naye Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Bw Daniel Mutani amekishukuru  Chuo Kikuu Mzumbe kwa mchango waliochangia  matibabu kwa watoto waliopo wodini lakini amesema  kuna watoto na wagonjwa wengine wanatibiwa matibabu ya nje hawapo wodini kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu, tunaomba muendelea kuwasaidia  wagonjwa hao pia. 


"Tunawashukuru  wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuchangia matibabu ya watoto. Lakini pia nawaomba msichoke muendelee na moyo wa kujitoa kwani  kuna wagonjwa wa nje wanahitaji msaada wa matibabu, naomba mtu yoyote au kikundi kuja kuwasaidia kwa uhitaji ni mkubwa”.. Amesitiza.


Pia tunaupokea Ushauri kuhusu kushirikisha wanafunzi katika kufanya tatiti tutaufikisha kwenye ngazi husika. “Kiukweli ni ushauri mzuri kwani ingawa kuna tafiti za kitabibu, lakini zipo zingine zinagusa jamii moja Kwa moja." Alisema Bw. Mutani
Awali muuguzi wa Wodi ya watoto wenye saratani Esteria Henjewele amesisitiza wazazi na walezi kuwafanyia  ukaguzi wa afya ya mara kwa mara watoto ili iwapo watagundulika na  tatizo waweze kuanfanyika matibau mapema kwani kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa saratani.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia Ndaki ya Dar es Salaam Bi Victoria Mnyanyi akitoa ukitambulisha Kaimu Mkuu wa Ndaki Dkt Coretha Komba na wanaju,iya wa chuo kikuu Mzumbe  kwa maafisa ustawi wa jamii hospitali ya muhimbili

No comments:

Post a Comment

Pages