HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 11, 2023

NBC YAIPIGA TAFU RIADHA AFRIKA MASHARIKI (EAAR)

NA TULLO CHAMBO, RT

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imelichangia Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Shilingi Milioni 3 katika mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki chini ya miaka 20 na 18 (EAAR Youth Championship), yanayofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Msaada huo ulitolewa na Mwakilishi wa NBC, Billygraham Minja na kupokewa na Makamu wa Rais wa RT, William Kallaghe.



Akizungumza baada kupokea msaada huo, Kallaghe, aliishukuru benki hiyo na kuelezea utasaidia kufanikisha ushiriki wa Tanzania kwani ndio safari imeanza.


"Tunashukuru sana kwa msaada huu na umefungua ukurasa mpya...NBC amekuwa mdau wa kwanza kutuchangia na tunaamini ushirikiano huu utaendelea," alisema Kallaghe na kuongeza.


Tunawakaribisha wadau wengine waige mfano huu wa NBC, tunapokea msaada wowote, kwani safari ndo imeanza, baada ya hapa tunakwenda Lusaka Zambia kwenye mashindano ya Afrika Aprili 27 hadi Mei 3.

No comments:

Post a Comment

Pages