HABARI MSETO (HEADER)


March 11, 2023

WAKAZI DAR WAJITOKEZA KUJISAJILI BRELA

Na Khadija Kalili, Michuzi TV
 

MSAIDIZI wa Usajili Brela Yvonne Maselle amesema  kuwa wakaazi wa Jiji la Dar Es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika kupata huduma za kusajili majina ya biashara zao.

Maselle amesema hayo leo Machi 10  ikiwa ni siku ya pili tangu Brela wawe mipngoni mwa mabanda ya Taasisi za Serikali yanayotoa huduma kwenye maonesho ya wajasiriamali na wafanyabiashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Msaidizi huyo wa Usajili Masele amesemakuwa kumekumekua na mwamko mkubwa kwa wananchi kufika kwenye banda la Brela na kujisajili.

"Tunamshkuru Mungu kwa muitikio hui waliouonesha japo itakuwa ngumu kwa sasa kutoa idadi ya waliojisajili ni kama unavyoona muda huu ni alasiri lakini bado watu wanaendelea kusongamana ili kupata usajili"amesema Masele alipizungumza na waandishi  wa habari.


Masele ameongeza kwa kusema kuwa Brela  wanaamini siku za mapumziko ambazo ni Jumamosi na Jumapili watananchi wengi watafika kupata huduma ya usajili huku akisisitiza kuwa wamejipanga vema kuwahudumia.


"Mbali ya kujisaliji pia tumekua tukitoa ushauri kwa mteja mmojammoja ili waweze kupata ufahamu zaidi ya kujisajili" amesema Masele.


" Hapa tunatoa huduma ya usajili wa Makampuni,Majina ya biashara, Alama za biashara.na Leseni za Viwanda .

No comments:

Post a Comment

Pages