HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2023

NCHIMBI MAMBO MAGUMU FOUNTAIN

Na Mwandishi Wetu

Mshambuliaji wa zamani wa Mabingwa Yanga SC Ditram Nchimbi bado analitafuta bao la kwanza tangu alipojiunga na Fountain Gate FC wakati wa dirisha dogo la usajili msimu huu.

Nchimbi tayari amecheza mechi tano (5) za Ligi ya Championship tangu ajiunge na Fountain Gate lakini bado mambo yamekuwa magumu kufumania nyavu za wapinzani   wala kutoa pasi ya bao ‘assist’.



Katika mechi tano (5) ambazo ameichezea Fountain Gate FC, ni mechi moja (1) tu ambayo alicheza kwa dakika zote 90! Mechi nyingine nne (4) aliingia akitokea benchi au alianza kwenye kikosi cha kwanza lakini alitolewa badae.

MECHI ALIZOCHEZA NCHIMBI FOUNTAIN GATE

1. Biashara United 1-0 Fountain Gate
2. COPCO 0-1 Fountain Gate
⚽️ Sadick Said
3. Fountain Gate 0-0 Mbeya Kwanza
4. Fountain Gate 1-1 Ken Gold
⚽️Daniel Joram
5. Fountain Gate 0-0 JKT Tanzania

Takwimu kwa msaada wa mtandao.


No comments:

Post a Comment

Pages