TAMWA-ZNZ yaanza mkakati mpya kushuka mashuleni kutoa elimu ya udhalilishaji
Zaidi
ya wanafunzi 300 kutoka shule mbili za wilaya ya mjini Unguja leo
wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na kutambua viashiria vya udhalilishaji
katika maisha yao ya kila siku.
Shule hizo ni Memon ya Stown
Town na Bubu ambapo maafisa wa TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na mitandao ya
kupinga udhalilishaji (GBV network) wamekuna na kutoa elimu kwa
wanafunzi hao kwa nyakati tofauti.
Wakati wakitoa elimu maafisa
hao wakiongozwa na afisa anashughulikia maswala ya udhalilishaji
TAMWA-ZNZ Zaina Salum amesema wameamua kuwafikia wanafunzi mashuleni
kutokana na sababu mbali mbali.
Alisema kwa kipindi kirefu
wamekua wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari jambo ambalo wanadhani
kuna wakati elimu hiyo haifiki kwa walio wengi na ndio maana kila leo
matendo hayo yamekua yakifanyika.
"Unajua ukija huku field ndio
haswa unakutana na watoto wenyewe ambao ndio wanaokumbwa na kadhia
hii,na hatuna hakika kutokana na umri wao kuwa wanaskiliza redio au
kusoma magazeti" aliongezea.
Pia aliwataka watoto hao kufanya
vitu muhimu ambavyo wanapaswa kuvifanya sasa kutoka na umri wao ikiwemo
kujikita zaidi katika elimu.
Mwawakilishi kutoka mtandao wa
kupinga udhalilishaji Huda Gharib aliwataka wanafunzi hao kuwa makini
sambamba na kuepuka makundi ya watu wasiowaamini hata mitaani mwao.
Pia
aliwataka wanafunzi hao kutoacha kabisa kuwa na aina ya marafiki
wasiokua wa umri wao kwani wanajua mambo mengi zaidi hivyo wanaweza
kuwashawishi.
Kwa nyakati tofauti watoto hao walioneshwa kuguswa na elimu hiyo na kueleza kuwa wanapaswa kuifanyia kazi.
Mmoja wao Saida Awadhi aliwataka watoto wenzake kutoa taarifa kwa wazazi wao pale wanapoona mazingira hatarishi kwao.
No comments:
Post a Comment