HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 08, 2023

TASAC yatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali ya Mtandao (eGA)

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma


Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), imebainisha kuwa inatekeleza miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini yanazingatiwa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Kaimu Abdi Mkeyenge leo Jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TASAC, pamoja na kubainisha Mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita.



Mkeyenge amesema kuwa TASAC imeunganisha ofisi zake zote zikiwemo zile za Mikoa, Wilaya na mipakani kwenye Mkongo wa Taifa ambao umerahisisha na kuharakisha mawasiliano ya ndani (Intranet), barua pepe, na mawasiliano na wadau wa nje .

Aidha ,Mkeyenge ameongeza kuwa uendelezaji wa miundombinu na mifumo ya TEHAMA ulianza mwaka wa fedha 2018/19 na utakamilika mwaka wa fedha 2025/26 huku mifumo ambayo inayoboreshwa ndani ya Shirika ni pamoja na mfumo wa ukaguzi, usajili wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji na utoaji wa vyeti vya Mabaharia (Maritime Administration Management System), mfumo wa utoaji leseni, ukusanyaji wa mapato ya udhibiti, uhakiki kadhia na kutoa ankara za malipo ya watoa huduma wa meli (Manifest Billing System), pamoja na mfumo wa kutoa huduma za biashara ya Meli.

 Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) imetusaidia katika kuhakikisha manunuzi, matumizi bora, sahihi na salama ya vifaa na mifumo yote ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini tunaitumia kwa mafanikio makubwa na tunaami mpaka mwaka wa fedha wa 2025/26 mifumo yote ndani ya Shirika itakuwa tayari,"


Pia Mkeyenge amesema katika kuimarisha usimamizi wa usalama, ulinzi na utunzaji wa mazingira dhidi ya shughuli za meli na kupunguza matukio ya ajali za vyombo vya majini TASAC imefanya sensa na kaguzi za vyombo vya usafiri majini ambapo kaguzi 6,208 katika mwaka wa fedha 2021/22 zilifanyika na kaguzi 4,490 zilfanyika katika kipindi cha Julai 2022 mpaka Januari 2023 inayotarajiwa kufikia vyombo takriban 8,000 ifikapo mwezi Juni 2023.

No comments:

Post a Comment

Pages