HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 12, 2023

WAFANYABIASHARA WAMESHAURIWA WASITUMIE MAJINA YA BIASHARA KABLA YA KUYASAJILI BRELA


Afisa Usaijili  Msaidizi BRELA, Bethod Bahanganoze, akiwa kwenye banda hilo akizungumza na waandishi wa habari.

Lucy Oisso (kushoto) akipokea cheti cha usajili kutoka kwa Afisa Tehama BRELA, Fadhili Mlosa baada ya kupata usajili wa jina la biashara kwenye banda hilo.


Na Khadija Kalili


WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA  wametoa rai kwa wananchi kuto kufanya biashara kwa kutumia majina bila ya kuyasajili kwenye  taasisi hiyo ya Serikali nchini ili kuepuka kupata changamoto za kupoteza wateja wao.


Yamesema hayo na Afisa  Usajili Msaidizi BRELA  Bethod  Bahanganoze wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari kwenye maonesho ya wajasiriamali na wafanyabiashara wanawake  yaliyofanyika kwa  siku ya tatu  kwenye viwanja  vya Mlimani City Jijini Dae  Es Salaam.

Bahangahanoze amesema kuwa wakiwa kwenye maonesho hayo wamewapokea wateja wengi ambao wamefika kujisajili huku wakipata changamoto ya kusajili majina ambayo wamekuwa wakiyatumia kwenye biashara zao na kukuta tayari yamesajiliwa lakini hapohapo wamekua wakiwapa ushauri wa kulazimika kubadilisha jina na wamefanikiwa katika hilo.


"Kutumia jina la biashara bila kurasimisha siyo sahihi pia ametaja kiwango cha kusajili jina la biashara ni 20,000 huku ada ya kulipia kila mwaka ni 5,000.

"Ila kiwango cha gharama cha usajili wa kampuni inatofautiana kitokana na ukubwa wa Kampuni.husika na kwa upande wa usajili wa alama za biashara tunasajili kwa 125,000  pia wanatoa huduma ya  kusajili uvumbuzi wa aina mbalimbali (Hataza) amesema Bangahanoze.

 
Wakati huohuo  Mteja Lucy Oisso wa Mbezi  Lois Jijini Dar es Salaam  ambaye amesajili BRELA amewashauri wafanyabiashara wenzake kutifanya makosa ya kutumia majina ya biashara bila kusajili BRELA kama yeye imemgharimu ametumia jina la biashara kwa miamka mingi bila kufanya usajili hivyo amelazimimika kubadilisha jina baada ya kukuta jina alilokuwa akilitumia limeshasajiliwa na mtu mwingine jambo ambalo amekiri litamsumbua  kwa muda katika biashara yake.

No comments:

Post a Comment

Pages