Na Victor Masangu, Kibaha
Mbunge
wa Jimbo la Kibaha mjini Silvesty Koka katika kuunga mkono juhudi za
Serikali ya awamu ya sita katika kuleta chachu ya maendeleo ameamua
kutumia fedha za mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kuboesha sekta ya elimu na
afya katika kata zilizopo pembezo mwa mji.
Hayo
yamebaibika wakati wa ziara ya kikazi kwa ajili ya kukagua na
kutembelea miradi mbali mbali ambayo imetekelezwa kwa kutumia fedha za
mfuko wa jimbo katika sekta mbali mbali ikiwemo miradi ya elimu pamoja
na afya.
Katika ziara
hiyo Mbunge huyo ameambatana na wajumbe wa kamati ya mfuko wa Jimbo
alisema lengo lake kubwa la kufa ya ziara hiyo ni kuweza kujionea jinsi
ya utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa fedha za mfuko wa
Jimbo.
Aidha
Koka alisema kwamba ataendelea kushirikiana bega kwa bega na wananchi
katika kusikiliza kero na changamoto ili kuweza kuzisikiliza na
kuzitafutia ufumbuzi lengo ikiwa ni kuwaletea mabadiliko chanya ya
kimaendelea katika nyanja mbali mbali.
"
Nia yangu kubwa ni kuwaletea maendeleo wananchi wangu wa Jimbo la
Kibaha mji,na ujio huu kikubwa ni kikagua fedha ambazo nimezitoa za
mfuko wa Jimbo zimefanya kazi yake ipasavyo na ndio maana nimeamua
kufanya ziara hii ili nione miradi imetekelezwa katika kiwango,"alisema
Koka.
Pia aliongeza kuwa
anataka kuona kata zilizopo pembezo zinapiga hatua kubwa ya kimaendeleo
na ataendelea kuwapambania wananchi wake ili waweze kupata fursa ya
kupata huduma mbali mbali za kijamii.
Katika
hatua nyingine aliwataka watendaji Kuhakikisha wanaweka mipango
madhubuti ya kutenga maeneo maalum ambayo yataweza kusaidia kwa kiasi
kikubwa katika kutumika kwa miradi ya maendeo kwa wananchi.
Kwa
Upande wao baadhi Diwani wa kata ya Mbwawa pamoja na diwani wa kata ya
Visiga wamemshukuru Mbunge huyo kwa kutenga fedha za mfuko wa Jimbo kwa
ajili ya maendeleo kwa wananchi wake.
Naye
mkuu wa shule ya sekondari misugusugu Mohamed Mwenda alisema juhudi
ambazo zimefanyika na Mbunge katika kusaidia viti 30 na meza 30 vimeweza
kuwa mkombozi mkubwa katika kusaidia wanafunzi kuondokana na adha ya
kukaa kwa msongamano.
Nao
baadhi ya wazazi na walezi wakiwemo viongozi wa chama wamempongeza
Mbunge huyo kwa kuwapambania kuleta chachu ya maendeleo katika sekta
mbali mbali pamoja na kutumia fedha za mfuko wa Jimbo katika miradi ya
maendeleo.
Mbunge koka amefanya ziara ya kishindo katika kata sita za Mbwawa.Visiga.Misugusugu, Kibaha,viziwaziwa
pamoja na Kibaha kwa ajili kutembelea miradi mbali mbali ambayo
baadhi yake imetekelezwa kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo.
No comments:
Post a Comment