HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 24, 2023

TIMU YA TAIFA RIADHA U 18&20 YAAGWA, MATUMAINI KIBAO

TIMU ya Taifa ya Riadha kwa vijana chini ya miaka   18 na 20, imekabidhiwa bendera ya Taifa leo Aprili 24 jijini Dar es Salaam, tayari kwenda kushiriki mashindano ya Afrika yatakayofanyika Ndola nchini Zambia Aprili 29 hadi Mei 3 mwaka huu.



Timu hiyo ilikabidhiwa bendera na Ofisa Michezo wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT), Charles Maguzu, aliyemwakilisha Katibu Mtendaji wa baraza hilo Neema Msitha.

Maguzu mbali ya kulipongeza Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), kwa maandalizi mazuri kwa timu hiyo ambayo ilikuwa kambini hosteli za Baraza la Maaskofu (TEC), Kurasini jijini Dar es Salaam toka Aprili Mosi, aliwataka vijana hao kujikita zaidi katika mchezo huo, kwani hivi sasa ni ajira tosha.

Maguzu, aliwataka kutambua kuwa, kwa kukabidhiwa bendera hiyo ya Taifa, kuna maana ya dhamana kubwa waliyopewa ya kwenda kuwapigania Watanzania zaidi ya milioni 60.

Naye Rais wa RT, Silas Isangi, aliwataka vijana hao kuondoa hofu na kwenda kupambana na kwa kufanya kwao vizuri, serikali itawatambua na kuwaenzi.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo,   Gasisi Gesasa, alisema wamejiandaa vema na wanakwenda kupambana.

Msafara wa timu hiyo ukiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAA), Muhidin Masunzu, unatarajiwa kuondoka alfajiri ya Aprili 25 kwa basi ukiwa na wachezaji 15, makocha wawili, meneja na daktari.

No comments:

Post a Comment

Pages