HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 24, 2023

CHUO KIKUU MZUMBE YAZINDUA KAMATI YA USHAURI WA VIWANDA CHINI YA MRADI WA HEET


 Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda ya Chuo Kikuu Mzumbe chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) jijini Dar es Salaam.

Kaimu Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda chini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.


Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Cyriacus Binamungu, akitoa neno la shukrani baada ya
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji, kuzindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda jijini Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam.
 

 

Na Mwandishi Wetu

 

CHUO Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation (HEET Project) unaofadhiliwa na benki ya Dunia kimezindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda kwaajili ya kuangalia mambo mbalimbali ili kuinua uchumi.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa "Kamati hiyo itaangalia mahusiano yapoje kati ya mazao yanayotoka katika taasisi za elimu ya juu na viwanda vyetu, wanafunzi wanatoka katika vyuo vyetu wanaendana na mahitaji yanayohitajika sokoni hasa kwenye viwanda vyetu.”

Amesema kuwa kumekuwa na kilio cha muda mrefu juu mahitaji ya soko ni tofauti na wanaozalishwa kutoka kwenye vyuo vyetu yaani wahitimu hawaendani na soko la ajira lililopo.
“Kuzinduliwa kwa kamati hii sasa kunakwenda kuiangalia kwa kina changamoto hii ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kati ya waajiri na waajiriwa.


Tunaamini tunakwenda kulifikia lengo kujibu changamoto hii ili kama tatizo lipo kwenye mitaala yetu tushughulike na mitaala ambayo italingana na mhitaji mhimu sokoni.

Akizungumzia kuhusiana na changamoto zilizopo kati ya waajiri na waajiriwa amesema kuwa Taasisi ya waajiri Tanzania (ATE) wamewahi kufanya utafiti mwaka 2011 hadi 2014 wakaja na ushauri kuwa mazao ya taasisi za elimu za juu haziendani na soko la ajira lililopo hasa viwandani.

“Lakini hata kwenye vikao tunavyokaa na sekta binafsi nao wanalalamika kuwa wanapowachukua wafanyakazi kutoka vyuo mbalimbali wanalazimika kwenda kuwapa mafunzo nje ya nchi ndio waje wafanyekazi waliyokusudiwa.” Ameeleza

Kwa upande wa Makamu Mkuu Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amesema chuo hicho kimepata dola za Marekani milioni 21 ili kutekeleza mradi huo, asilimia 80 na fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa miundombinu na asilimia 20 ni kwaajili ya kutekeleza mambo mengine ikiwemo kuendeleza wanataaluma.

Amesema kuwa katika kutekeleza mradi huo wataanzisha mbinu bunifu za kufundishia ikiwa ni pamoja na kuboresha mitaala ya kufundishia na kujenga ushirikiano na Sekta ya viwanda pia kuwa na atamizi ya kuwanoa wataalamu mbalimbali watakaoenda kufanya kazi katika viwanda hapa nchini.

“Ili kutatua changamoto ya ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko na uchumi wa sasa kwa wahitimu wetu, sisi Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), tumedhamiria kujenga muunganiko imara katika ya elimu ya juu na viwanda. Kupitia mradi huu tunatazamia kuwa tutajenga mashirikiano, ubia, na kuendesha shughuli za pamoja na viwanda ambazo zitawawezesha wanafunzi na wafanyakazi kupata ujuzi na uzoefu kupitia kushughulika na changamoto halisi zinazotokea katika viwanda na soko la ajira.” Amesema Prof. Mwegoha.



Kwa upande wa mwakilishi wa Wanafunzi na Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe, amesema kuwa wataenda kuyafanyia kazi maelekezo waliyopewa ikiwa ni pamoja na kujifunza kwa bidi ili kuendeleza taifa kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment

Pages