HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 26, 2023

CRDB yashiriki mapokezi ya Mwenge Kigamboni


 

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni (kushoto), Halima Bulembo, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Munkunda (kulia) kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya hiyo ambapo jumla ya miradi sita imekaguliwa. Wa pili kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Abdallah Kaim.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulimbo, akiushika Mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Abdalah Kaim kabla ya kukimbizwa na kuzindua miradi ya mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akiushika Mwenge wa Uhuru kabla ya kukimbizwa na kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Benki ya CRDB.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Munkunda (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, wakati wa sherehe za kukabishi Mwenge Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni. 

 Meya wa Temeke, Abdallah Mtinika (katikati) akipeana mkono na Meneja wa CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd.

No comments:

Post a Comment

Pages