HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 27, 2023

Benki ya CRDB yadhamini mbio za Mwenge wa Uhuru 2023

 

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kushoto) kwa ajili ya kukimbizwa na kukagua miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo leo Mei 27, 2023. Mbio hizo zimedhaminiwa na Benki ya CRDB.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashim Komba akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mmoja wa vijana wakimbiza Mwenge Kitaifa 2023 Emmanuel Jackson kabla ya kuanza kukimbizwa na kukagua miradi saba ya maendeleo katika wilaya hiyo. 

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akipokea mwenge kutoka kwa mmoja wa vijana wakimbiza Mwenge Kitaifa Emmanuel Jackson wakati wa mapokezi wa Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ubungo ukitokea Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei 27, 2023. Benki ya CRDB imedhamini mbio hizo katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.


Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Hisia Theatre cha jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wa kucheza na nyoka wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Ubungo.


No comments:

Post a Comment

Pages