Kutoka kushoto Diwani wa Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lidya Mgaya anayefuata Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mama Selina Koka akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambarage Happiness Msaki na Mjumbe Kamati ya Siasa Catherine Katele (Mwenye Suti) wengine wanaoshuhudia ni Diwani Kata ya Tumbi Kibaha Raymond Chokala na Asha Baraka.
Na Khadija Kalili
MKE wa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mkoani Pwani Bi Selina Koka ameahidi kuandaa harambee maalumu itakayochangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nane ikiwa ni katika kutatua changamoto za upungufu wa madarasa Shuleni hapo.
Mama Koka amesema hayo leo Mei 29 asubuhi alipofika Shuleni hapo kwa ziara maalumu na kuweza kujionea hali halisi jinsi ilivyo huku akiwa ameambatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Diwani wa Kata ya Tumbi Mheshimiwa Raymond Chokala,Mjumbe Kamati ya Siasa Catherine Katele na wadau wengine mbalimbali wa masuala ya Siasa akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,MNEC Mstaafu Asha Baraka.
Mama Koka ameshiriki katika uchangiaji mpango wa kunywa uji Shuleni hapo ambapo pia ametoa sukari mifuko 20 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza pia ametoa katuni 180 ambazo waligaiwa wanafunzi wa darasa la kwanza shuleni hapo.
Akizungunzia kuhusu harambee hiyo Mama Koka amesemakuwa wataunda Kamati maalumu ambayo itaratibu namba ya uchangi
shaji wa fedha za ujenzi wa madarasa ambayo yatakwenda sanjari na ukarabati wa madarasa yaliyochakaa huku yeye ameahidi kukarabati darasa la wanafunzi wa darasa la awali.
Aidha Mama Koka amesema kuwa Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini ameahidi kununua madawati 70 kati ya 140 ambayo yanahitajika shuleni hapo.
"Wakati huohuo Mke wa Mbunge huyo ametoa wito kwa wazazi wa wanafunzi hao kujijengea mioyo ya kuchangia masuaala mbalimbali ambayo yataleta maendeleo katika Shule huku akiwaambia msirudi kwenye uchangiaji mkisikia kuna michango ya 1,000 au 2,000 changieni ili na sisi tukija pamoja na Viongozi wengine na kuona mwamko wenu katika uchangiaji mnatupa moyo zaid i wa kujitolea" amesema Mama Koka.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambarage Happines Msaki amesema kuwa shule hiyo inachangamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kukosa uzio jambo ambalo huchangia kukosesha usikivu kwa wanafunzi shuleni hapo.
Wakati huohuo Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani ameongea kwa uchungu madhila yanayowakuta baadhi ya wanafunzi Shuleni hapo "Nawaomba wazazi muwe walinzi wa wanafunzi hawa ambao ni watoto wetu jambo hili la ukosefu wa maadili nalizungumza kwa uchungu mwingi,suala la ukatili wa kijinsia katika Kata hii ya Tumbi Shule hii tunaongoza kwa vitendo hivi viovu kwani kuna kesi 20 na nyingi ni za shuleni hapa ,hivyo nauomba uongozi wa Shule tushirikiane pamoja katika haya mapambano na sisi Viongozi wa Kata ya Tumbi tumejipanga vizuri na hizo kesi ambazo tayari ziko Polisi tunazifuatilia kwa ukaribu wa hali ya juu si sahihi kuwaharibia watoto maisha hii ni dhambi kubwa huku watendaji wa vitendo hivyo wakiwalaghai kwa kuwapa chip's, chocolate na kuwabaka hili jambo halikubaliki"amesena Diwani huyo wa Tumbi Chokala.
No comments:
Post a Comment