Afisa Mkuu wa wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Alfred Shayo (kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 200 iliyotolewa kwa ajili ya udhamini wa Mkutano wa 37 wa ALAT unaofanyika Arusha. Anayepokea hundi ni Makamu Mwenyekiti wa ALAT, Sima Constatin na wengine ni baadhi ya maafisa waandamizi wa Benk ya NMB na pia kutoka ALAT. Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Praygod Mphuru (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya Biashara za Serikali wa NMB,Vicky Bishubo (wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita, Zahara Michuzi na Katibu wa ALAT Taifa, Mohamed Maje (wa pili kulia). (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya NMB imebainisha utayari wake wa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na
serikali za tawala za mitaa, ikiwemo kufadhili mikutano ya kila mwaka
ya Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT).
Dhamira
ya kudumisha ushirikiano huo iliwekwa bayana jana jijini Arusha na
benki hiyo wakati inatangaza ufadhili wa TZS milioni 200 wa mkutano mkuu
wa 37 wa ALAT ambao umeanza rasmi leo hii.
Wakizungumza
kabla ya kutangazwa kwa udhamani wa mwaka huu kwenye Ukumbi wa AICC,
viongozi waandamizi wa NMB walisema hii ni mara ya saba kwa taasisi yao
kufanya hivyo.
Afisa
Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Bw Alfrded Shao, alisema udhamini
walioufanya ndani ya kipind hicho sasa umefikia zaidi ya TZS bilioni
1.2.
“Tuna
miaka zaidi ya saba pamoja na ALAT katika masuala ya maendeleo ya taifa
letu na ndio maana wenzetu walipotufuata tuwaunge mkono hatukusita hata
kidogo,” alibainisha.
“Hata
hivyo, kubwa zaidi leo tunatangaza ushiriki wetu kama mdhamini wa
Mkutano Mkuu wa ALAT kwa kiasi cha TZS milioni. 200 ilikufanikisha
mkutano huu,” aliongeza na kusema wamekuwa wakishirikiana na ALAT hasa
kusaidia kuboresha miundombinu ya elimu, afya, usafiri na mazingira
kupitia wananchama wake ambao ni halmashauri 184 nchini kote.
Aidha,
Bw Shao aliitumia hafla ya kukabidhi hundi ya udhamani wa mwaka huu
kuonyesha jinsi NMB inavyozihudumia halmashauri, serikali kuu na taifa
kwa ujumla hasa kupita huduma zake bunifu za kifedha.
Alisema
moja ya maeneo ambayo wamefanikiwa katika hilo ni kurahisisha
ukusanyanji wa kodi kupitia mifumo bora inayowezesha Serikali ya Awamu
ya Sita katika kukusanya mapato yake.
“Ubunifu
na uwekezaji ambao tumeufanya kwenye teknolojia ulituwezesha kuwa benki
ya kwanza kuunga mifumo yetu na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya
Serikali (GePG) na hadi sasa zaidi ya taasisi 1,100 tayari zimeunga
mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato,” kiongozi huyu
alibainisha.
“Kwa
mfano, kupitia mifumo yetu mbalimbali ya malipo tumewezesha Serikali
kukusanya TZS trilioni 8.6 kupitia GePG kwa miaka mitatu kuanzia mwaka
2019 hadi 2021,” aliongeza kusema akisisitiza kuwa fedha hizi
zilikusanywa kupitia mifumo ya kidijitali kama NMB Mkononi, NMB Wakala
na hata internet banking.
Kauli
mbiu ya mkutano mkuu wa ALAT wa mwaka huu ambao ni wa siku tatu ni:
“Uboreshaji wa Miundombinu ni Chachu ya Utoaji wa Huduma Bora katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa”.
Makamu
Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Bw Sima Costantine Sima, aliipongeza NMB kwa
kusaidia kuboresha upatikanaji wa huduma hasa zile za kifedha nchoni
lakini pia mchango wake katika kuendeleza ustawi wa jamii.
Alisema
ALAT na wananchama wake 184 wanathamini ushirikiano wao mzuri wa
kibiashara na kimaendeleo na benkii hiyo ambao umekuwa ni wa manufaa kwa
wao wote pamoja na wananchi wanaowahudumia.
No comments:
Post a Comment